Monday, April 1, 2013

BABA TEGETE ASEMA NGUMI YA JULIO ALIYERUSHA NI SHABIKI, AELEZA ALIVYOKWENDA HOTELINI WALIKOFIKIA SIMBA








Lile sakata la Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kupigwa ngumi limezidi kushika kasi baada ya Kocha Mkuu wa Toto African, John Tegete kukataa katakata kwamba mchezaji wake amehusika.


Tegete ambaye ni baba mzazi wa mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete amesema Julio alipigwa ngumi na shabiki na wala si kiungo wake, Emmanuel Swita.


Akizungumza na Salehjembe, Tegete alisema shabiki ndiye alimpiga ngumi Julio baada ya kuzuka kwa tafrani.


“Unajua Julio alitoa ufunguo wa gari letu akidai kwamba kuna mpira ndani ya basi letu, alitaka urudishwe.



“Mimi nilimhakikishia hakukuwa na mpira, lakini aliendeleza mzozo na shabiki mmoja ambaye alikuwa amevaa nguo za kawaida alimpiga ngumi Julio, si mchezaji yoyote wa Toto.



“Unajua mimi niliona kama ana makosa, nafikiri haikuwa sahihi yeye kwenda kugombea mpira, angemuacha kit manager akafanya kazi hiyo.


“Hata hivyo baadaye nilikwenda katika hoteli waliyokuwa wamefikia, nikazungumza naye. Ninaamini atakuwa ameelewa kila kitu,” alisema Tegete na kuongeza.


“Unajua hata Julio alikuwa na makosa yake, lakini nakuhakikishia siwezi kusema eti namficha mchezaji wangu kama kweli angekuwa amempiga Julio.”


Julio amekuwa akisisitiza kwamba alipigwa na kiungo wa Toto Emmanuel Swita wakati wa purukushani hizo wakati akimdai mpira baada ya mechi kati ya timu hizo kumalizika kwa sare ya bao 2-2 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.


Tayari Julio ameapa kulipiza kisasi katika hilo, huku akimshutumu Tegete pamoja na daktari wa Toto African kwamba walikuwa wakijua kila kilichokuwa kikiendelea ikiwemo na mbinu za kutaka kuuiba mpira wa Simba.

chanzo saleh -jembe

Tags: ,

0 Responses to “BABA TEGETE ASEMA NGUMI YA JULIO ALIYERUSHA NI SHABIKI, AELEZA ALIVYOKWENDA HOTELINI WALIKOFIKIA SIMBA ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI