Tuesday, April 2, 2013
DC ASHAURI ‘NIACHE NISOME’ IWE TAASISI KUWALINDA WASICHANA KIELIMU
Tuesday, April 2, 2013 by Unknown
MKUU wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu ameshauri kampeni aliyoianzisha wilayani humo yenye kauli ya ‘Niache Nisome’ kupambana na mimba kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa elimu, iwe taasisi na kufanya shughuli zake nchi zima.
Rweyemamu aliyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi juu ya hali ilivyo kwa sasa ya matukio ya mimba kwa wanafunzi na kukatishwa masomo, vitendo ambavyo alivikuta vikishamiri eneo hilo hasa mwanzoni mwa mwaka jana kabla ya uteuzi wa nafasi hiyo.
Akizungumzia kampeni ya ‘Niache Nisome’ aliyoianzisha muda mfupi baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuiongoza wilaya hiyo, alisema kampeni yake imekuwa na mafanikio kwani licha ya matukio ya mimba kupungua wananchi wameipokea vizuri kampeni hiyo.
Alisema wananchi hasa baadhi ya wazazi wamekuwa wakiripoti matukio ya mimba na kutoa ushirikiano pale inapoitajika ili wavunjaji sheria kwa wanafunzi waweze kuadhibiwa kitendo ambacho hapo awali kilikuwa kigumu, na hata wengine kushirikia mikakati ya kuwaachisha masomo wanafunzi.
“Nina furahi kuwa muitikio wa kampeni ya ‘Niache Nisome’ katika maeneo mengi ya wilaya yangu imepokelewa vizuri, wananchi wanaanza kutambua umuhimu wa elimu na wanatoa ushirikiano kwa wale wachache wanaokwenda kinyume kwa kuwakatisha masomo wanafunzi hasa wa kike…jamii ya hapa wengi wao mwanzoni ilikuwa ni kitu cha kawaida mwanafunzi kulala nje pasipo idhini ya wazazi wake,” alisema Rweyemamu akizungumza.
This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DC ASHAURI ‘NIACHE NISOME’ IWE TAASISI KUWALINDA WASICHANA KIELIMU ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.