Thursday, March 21, 2013

AIRTEL YAZINDUA GHARAMA NAFUU ZAKUPIGA SIMU MITANDAO MINGINE







…………………………………………………………………..


Dar Es Salaam Jumatano 20 Marchi 2012. Airtel Tanzania leo imezindua
huduma mpya ijulikanayo kama “AIRTEL YATOSHA” itakayowawezesha wateja
wake nchi nzima kupiga simu kwenda mtandao wowote kwa kiwango nafuu
cha hadi asilimia 75 bila kuwa na sababu kubadili simu laini kwa
kuhofia gharama.
Huduma ya AIRTEL YATOSHA inadhihirisha simu kadi moja, taifa moja, bei
moja inayoendeleza dhamira ya Airtel ya kutoa huduma bora na nafuu
ambapo wateja wa Airtel sasa watapata ofa ya kifurushi kitakacho wapa
muda wa maongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet ambacho
kinaweza kutumika kwa siku au kwa wiki kulingana na mahitaji ya wateja


Akiongea wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa huduma hiyo iliofanyika
katika makao makuu ya Airtel Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw
Sunil Colaso Alisema” Huduma ya Airtel YATOSHA ni maalum kwa kila
mtanzania, hii itawarahisishia watanzania wote kupata mawasilino
nafuu kwa kupiga bila kikomo kwenda mitandao mingine nchini. Kupitia
kifurushi cha Airtel YATOSHA wateja wa Airtel watafurahia kiwango cha
chini cha hadi shilingi 349/=, hii inamaana kwamba mteja atapata
dakika 10 za kupiga simu kwenda mtandao wowote muda wowote, pia SMS
100 (ujumbe mfupi wa maneno) pamoja na kifurushi cha intenet cha 25MB
ofa itakayotumika masaa 24 kwa siku


Faida za AIRTEL YATOSHA kwa mteja zinadhihirisha dhamira yetu Airtel
ya kutoa huduma za mawasiliano bora na nafuu nchini. Airtel
tunazingatia kuwa wateja wetu wanamahitaji tofauti na ndio sababu
kubwa inayotufanya tuwe wabunifu kwa kuwapatia huduma zinazogusa kila
aina ya wateja na kuleta mabadiliko halisi kwa kuwapa wateja wetu nchi
nzima thamani ya pesa zao


Tags: ,

0 Responses to “AIRTEL YAZINDUA GHARAMA NAFUU ZAKUPIGA SIMU MITANDAO MINGINE ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI