habari mpya
Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts

Sunday, March 30, 2014

MASHALI AMPIGA KASEBA KWA POINTI

Sunday, March 30, 2014 - by Unknown · - 0 Comments




 
Bondia Thomas Mashali (kushoto) akikwepa konde la Japhet Kaseba, wakati wa pambano lao kuwania Ubingwa wa WBO uliofanyika kwenye ukumbi wa UBO Africa Mashali. Sabasaba jijini Dar es Salaam. Katika pambano hilo Mashali alimshinda mpinzani wake kwa Pointi.

Saturday, March 29, 2014

KASHFA YA USHOGA YAMTESA ASHLEY COLE..AKUNUSHA

Saturday, March 29, 2014 - by Unknown · - 0 Comments




 
MAPEMA wiki iliyopita uvumi ulisambaa nchini England kwamba gazeti maarufu la The Sun lilikuwa mbioni kuchapisha stori ndefu iliyohusu kashfa ya ushoga ya mlinzi mmoja wa sasa wa kushoto wa timu ya taifa ya England.

Hata hivyo, Gazeti la The Sun la juzi Jumapili lilikanusha kutaka kuandika stori hiyo, lakini bado mlinzi wa kushoto wa England na Chelsea, Ashley Cole akawahi kukanusha kwamba alikuwa hahusiki na kashfa hiyo.

Cole ameimiliki nafasi ya ulinzi upande wa kushoto tangu Machi 2001 na ndiye mchezaji wa pembeni aliyecheza mechi nyingi zaidi katika kikosi cha timu ya taifa ya England.

Na kama kutakuwa na ukwlei wowote katika habari hiyo ni wazi kwamba hilo litakuwa pigo jingine kwa mchezaji huyo ambaye kwa sasa anahaha kupata namba hiyo hiyo aliyoitawala muda mrefu katika kikosi cha Chelsea na hivyo hiyo kuwa nuksi nyingine inayomuandama mchezaji huyo.

Mashabiki wengi waliamini kwamba Cole alikuwa anahusika na kashfa hiyo.

Mwingine aliyeonekana kuhisiwa katika kashfa hiyo ni mlinzi kinda, Luke Shaw ambaye ameanza kuichezea timu ya taifa ya England katika pambano la kirafiki dhidi ya Denmark Machi 8 mwaka huu. Hata hivyo wote wawili wametumia mitandao yao ya mawasiliano kukanusha uwepo wa habari hiyo.

Cole aliandika katika mtandao wake akisema ‘strictly chicks only’, akimaanisha anapenda wasichana tu, wakati Shaw aliandika kwa kusema ‘Si mimi’. Cole alikuwa katika ndoa na mwanamuziki maarufu wa Kundi la Girls Aloud, Cheryl Cole ambaye pia aliwahi kuwa jaji wa michuano ya kusaka vipaji ya X Factor lakini ndoa yao ikavunjika mwaka 2010 kutokana na kile kilichodaiwa kuwa Cole hakuwa mwaminifu katika ndoa hiyo.

Uvumi ulitanda Jumamosi usiku iliyopita katika mitandao ya kijamii kwamba The Sun la Jumapili lingemtaja mchezaji mmoja katika kikosi cha kocha Roy Hodgson ambaye anahusika na kashfa ya ushoga.

Kama gazeti hilo lingefanya hivyo, huyo angekuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya timu ya taifa ya England kujitangaza kuwa shoga. Hata hivyo gazeti hilo lilikanusha waziwazi kwamba stori hiyo ilikuwa imepikwa na watu wasiojulikana.

Huo ni mwendelezo wa habari za ushoga zikuibuka katika vyombo vya habari vya Uingereza baada ya staa wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani, Thomas Hitzlspelger kujitangaza kuwa shoga Januari mwaka huu.

Nyota huyo wa zamani wa Aston Villa, Everton na West Ham amekuwa mchezaji wa kwanza wa Ligi Kuu England katika mfumo mpya kujitangaza kuwa shoga.

KASEJA AMHENYESHA DIDA YANGA

- by Unknown · - 0 Comments




 
UMAHIRI wa kipa, Juma Kaseja na Ally Mustapha ‘Barthez’, umemhenyesha Deo Munishi ‘Dida’ ambaye analazimika kukesha mazoezini ili asichuje.

Dida ametamka kuwa ubora wa makipa hao unamfanya afanye kazi ya ziada ambayo anahisi hakuwahi kuifanya katika klabu nyingine zote alizowahi kucheza, pia anaogopa kupigwa benchi na Kaseja kama enzi hizo walipokuwa Simba pamoja.

Kiwango cha Dida kimeimarika kwa sasa na mwenyewe anasema: “Ubora wangu umeongezeka na kuwa juu kwa sababu ya uwepo wa Kaseja na Barthez, ni makipa mahiri kwenye ligi.

“Kwa sababu ya ubora wao, inanifanya nisibweteke, nijitume ili niwe bora zaidi na zaidi. Kama nitabweteka na kuwa chini ya kiwango hata kidogo tu, ni wazi sitapata namba.

“Lakini kama ningekua nacheza kikosi kimoja na makipa wengine wasio na uwezo, lazima ningebweteka kwa sababu ningekosa ushindani na kiwango kingebaki kama kilivyo kwa kukosa changamoto.”

Dida anatarajia kuanza mazoezi mwishoni mwa wiki hii, alikuwa kwenye mapumziko akiuguza kidonda kwenye bega la kushoto.

Alijikata na geti nyumbani kwake, lakini aliibua tatizo lingine baada ya kupakaa dawa ya spiriti nyingi iliyomuunguza na kusababisha kidonda hicho kuongezeka. Yeye amesisitiza anaendelea vizuri na atarudi uwanjani akiwa na kasi hiyo hiyo.

DAVID MOYES AJITETEA ..."HATA INGEKUWA NI FERGUSON MSIMU HUU ANGEPATA WAKATI MGUMU"

- by Unknown · - 0 Comments


Meneja wa klabu ya Manchester United, David Moyes amedai kwamba msimu huu wa kwanza kwake hata ungekuwa kwa Sir Alex Ferguson angepata shida kufanya la maana ndani ya msimu ukilinganisha na wachezaji wake wenye umri mkubwa.

 
“Ukweli nadhai kwamba kama Sir Alex angekua hapa mwaka huu ingekua ngumu kwa Sir Alex pia,nina uhakika hata yeye analijua hilo. Nafikiri watu wanatambua kwamba kuna kikosi ambacho kimepita umri, kwa maana hiyo nadhani ingekua ni msimu mgumu labda kwa yeyote ambaye angekabidhiwa Manchester United mwaka huu,” alisema Moyes

Kauli hiyo ya Moyes imekuja huku Jumamosi hii kundi la mashabiki wa Manchester United likipanga kukodisha ndege itakayopeperusha kibendera chenye maandishi ya kumpinga kocha huyo. Manchester United imekuwa na msimu mbaya kiasi cha mashabiki wa timu hiyo kuanza kulalamika vikali wakimtaka Moyes afutwe kazi.

Wednesday, March 26, 2014

YANGA NA AZAM WAZIDI KUKABANA KOO..WOTE WASHINDA LEO

Wednesday, March 26, 2014 - by Unknown · - 0 Comments



 
Vilabu vya Azam FC na Yanga SC leo vimeendelea kukabana koo katika mbio za ubingwa wa ligi kuu Vodacom baada ya vyote viwili kupata ushindi kwenye michezo yao waliyokuwa wakicheza leo hii.
Azam FC ikiwa katika dimba la Mkwakwani ilikuwa ikicheza na Mgambo JKT na matokeo ni kwamba wamefanikiwa kushinda kwa magoli 2-0.
Magoli ya Azam yalifungwa na Brian Omony na John Bocco Adebayor.
Kwa upande wa Yanga ambao leo walikuwa wakicheza na Tanzania Prisons kutoka Mbeya katika uwanja wa taifa – matokeo ni Yanga wameshinda 5-0.
Magoli ya Yanga yalifungwa na Emmanuel Okwi, Mrisho Ngassa, Hamis Kiiza alifunga mawili na nahodha Nadir Haroub Cannavaro aliyefunga kwa penati.

MASHABIKI WA MAN U WAELEKEZA HASIRA ZAO KWA MOYES NA ALEX FERGUSON

- by Unknown · - 0 Comments





Shabiki akimtukana David Moyes
Kichapo cha bao 3-0 walichopata jana kutoka kwa Manchester City kimewakasirisha mashabiki wa Manchester United, na wameamua kuelekeza hasira zao kwa kocha Davidi Moyes na Sir Alex Ferguson.

Shabiki akimtukana David Moyes

Kufungwa huko kulipandisha hasira za mashabiki wa timu hiyo ambapo wale waliokuwa karibu na David Moyes walilazimika kushikwa na walinzi wakitaka kumshambulia huku wengine wakielekeza hasira zao kwa Ferguson.

Mashabiki wanalaumu uamuzi wa Ferguson kumwachia mikoba Moyes kama kocha wa Manchester United.

Monday, March 24, 2014

SANAA HAILIPI, WENGI WANAISHI MAISHA YA KUIGIZA!

Monday, March 24, 2014 - by Unknown · - 0 Comments


SOKO la filamu limekua, maisha ya vijana wengi yamebadilika kutokana na sanaa hiyo. Hata hivyo bado kuna changamoto kadhaa; malipo ya wasanii na mikataba mibovu imeendelea kuwa kilio kwao.
Hilo linawafanya waendelee kubaki palepale licha ya kupanda kwa hatua nyingi takriban miaka saba iliyopita. Sinema kwa sasa, imebaki kuwa na manufaa zaidi kwa msambazaji badala ya msanii ambaye kimsingi ndiye mhusika mkuu katika utayarishaji.

Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba amefafanua mengi kuhusu changamoto zilizopo katika sanaa hiyo.

WANASOKA WA AFRIKA WASAMBAA KILA KONA DUNIANI

- by Unknown · - 0 Comments



 
Ni hali ambayo imekuwa kama kawaida kwa wachezaji wa Afrika kutafuta kwenye klabu mbalimbali barani Ulaya.

Kutokana na hali ya uchumi iliyopo katika nchi za Afrika, kijana anayecheza soka kwenye viwanja vyenye vumbi kwa sababu ya kukosekana viwanja bora hujikuta akiwa na ndoto ya kujiendeleza kucheza soka nje ya Afrika ili aweze kufanikiwa kimaisha kwa kutumia kipaji chake.

Lakini wakati wachezaji wengi wa Afrika wakiwa na ndoto za kucheza soka katika Ligi Kuu za England, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Ureno na Hispania, ripoti iliyotolewa na Shirikisho la Soka Kimataifa (FIFA) hivi karibuni inaonyesha wachezaji wa Afrika wamezidi kumiminika sehemu mbalimbali za dunia kutoka Albania hadi Yemen kwa ajili ya kutafuta ‘malisho’.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya FIFA, katika kipindi cha miaka 25 iliyopita, ukiacha nchi zilizokuwa zikitamba kisoka barani Ulaya, wachezaji wa Afrika wameingia mpaka katika nchi za Ulaya ambazo zilikuwa hazitambi kisoka.

Ripoti hiyo inaonyesha katika miaka ya 1990 wachezaji wa Afrika walikuwa katika timu kubwa tu za Ulaya zinazoshiriki kwenye ligi za juu za nchi, lakini hivi sasa wachezaji wa Afrika wamesambaa mpaka kwenye ligi mbalimbali za chini.

FIFA inasema idadi ya wachezaji wa Afrika itaendelea kuongezeka barani Ulaya. Pia wachezaji wa Afrika wana nafasi kubwa nje ya bara la Ulaya na sasa wengi wapo katika Ligi Kuu ya Marekani, Vilevile wapo katika nchi za Mashariki ya Kati wanacheza soka na kunufaika na fedha zinazotokana na mauzo ya mafuta.

Ukitazama Ligi ya Mabingwa Asia, msimu uliopita kulikuwa na wachezaji wengi wa kiafrika kwa sababu wanacheza soka katika ligi mbalimbali za bara hilo kama ligi ya India, Indonesia, China na nyingine nyingi.

Katika hali ya kushangaza, taarifa ya FIFA inaonyesha wachezaji wa Afrika ni wachache katika Ligi ya Mabingwa ya Amerika ya Kusini.

Monday, March 17, 2014

MOYES AONDOKE MAN UNITED - NA HIZI SABABU KWANINI HAFAI KUENDELEA KUIFUNDISHA KLABU HIYO

Monday, March 17, 2014 - by Unknown · - 0 Comments





Manchester United lazima imtimue David Moyes mwishoni mwa msimu huu. David Moyes hana uwezo wa kuiongoza Manchester United kuendeleza mazuri ya aliyemrithi na kuipeleka timu kwenye kilele cha mafanikio, jambo ambalo ndilo linalotegemewa katika klabu ya ukubwa wa United. Badala ya kuendelea uongozi mbovu wa Moyes, klabu inabidi ubora na uimara wa timu kupitia kocha na benchi la ufundi ambalo huko nyuma tayari wameshaongoza timu kwa mafanikio. United ina ufuasi mkuwa wa mamilioni ya mashabiki duniani kote na kutokana na hili United inastahili kupata uongozi bora zaidi kuliko huu wa Moyes.

Sababu kwanini Moyes aondoke Manchester United:

Kukosa uzoefu wa kushinda - Moyes hajawahi kushinda kombe katika career yake ya ukocha - ukiondoa kombe la nguo la hisani, ambalo alikuta timu yake imeshafikishwa kwenye mchezo huo tena dhidi ya timu ya ligi ya daraja ya kwanza ya Wigan.

Ukosefu wa uwezo wa kufundisha wachezaji wakubwa - Ukweli wa kwamba hajawahi kuwa na bahati ya kuwa na kikosi chenye wachezaji wakubwa unamaanisha kwamba hajui namna nzuri ya kudili na aina ya wachezaji wa aina hiyo, kuwafurahisha na kuwapa motisha au kujua namna ya kupata kiwango kilicho bora kutoka kwao. Ni vigumu kutegemea wachezaji walioshinda kila kitu na matajiri kumheshimu kocha ambaye hajawahi kushinda kitu chochote.

Ukosefu wa uzoefu wa kudili na mategemeo makubwa - Baada ya kuwa Everton kwa miaka 11, mahala ambapo alikuwa akifaulu kumaliza ligi katikati mwa msimamo akiwa na bajeti ndogo ya usajili, Moyes hana uzoefu wa kudili na presha ya mategemeo makubwa ambayo huja pamoja na kazi yake ndani ya United - na hilo tayari limeshaonekana.

Mbinu zilizopitwa na wakati - Ukosefu wake wa mbinu bora mwanzoni na kati kati ya mchezo zimeigharimu sana timu msimu huu. Baada ya mechi ya Fulham Rene Maulesteen alisema ilikuwa kazi rahisi sana kucheza na United yenye mbinu zilezile zilikosa mabadiliko, pia beki wa kati wa Fulham Dan Burn alizidharau mbinu za Moyes kwamba zilikuwa rahisi sana kuzuia. Akiichezesha timu kwa mfumo wa kizamani 4-4-2 - timu haionyeshi kuwa na maendeleo bora katika kipindi cha miezi tisa ya utawala wake, lakini pamoja na haya yote bado haonekani kulitambua tatizo hili la mfumo na kulitafutia ufumbuzi.

Wasaidizi wabovu - Makocha wasaidizi wa United chini ya Sir Alex walikuwa Meulensteen, Mike Phelan na Eric Steele. Wote kwa pamoja walikuwa na uzoefu wa ukocha wa level ya juu kwa miaka 25 na walikuwa walikuwa wanajua namna ya kuwaandaa vijana kushinda mechi na kushinda makombe. Uamuzi wa Moyes kuwaondoa hawa wasaidizi umezidi kuwa mbovu baada ya kuwaleta wabadala wao: Phil Neville (hakuwa mchezaji wa daraja la juu, hana uzoefu mzuri wa ukocha zaidi ya kuhusika na timu ya England U21, ambayo ilikuwa ikifanya vibaya), Steve Round (alikuwa mmoja ya makocha walioishusha timu mpaka daraja la kwanza kutoka EPL, hana uzoefu wa kufundisha timu kubwa), Ryan Giggs (mchezaji wa daraja la juu - lakini ni kocha ambaye hana uzoefu), na Moyes mwenyewe (mbinu zake hasi - anaendekeza zaidi mazoezi magumu badala ya mazoezi ya kiufundi). Je watu hawa wana uwezo na wanafaa kuliongoza benchi la ufundi na kupata kilicho bora kutoka kwa wachezaji wa hadhi ya juu, na kwa mtazamo wa sasa inaonekana jibu ni hapana, wameishindwa kazi hiyo.

Namna mbovu ya kudili na vyombo vya habari - Namna Moyes anavyodili na vyombo vya habari tangu sio sawa kabisa tangu alivyofika Old Trafford. Hana approach nzuri - Amekuwa akisisitiza kwenye jibu moja kwamba timu ina "bahati mbaya" na kurudia rudia msemo wake wa "Nadhani tumecheza vizuri" (Timu iwe imefungwa, imeshinda, au suluhu) - hii kauli inaonyesha ambition. Manchester United inabidi isiwe na mtazamo wa kukubali suluhu au vipigo kwa namna Moyes anavyochukulia. Inabidi tutegemee ujuzu, mbinu, na nguvu katika kutafuta ushindi kuliko kutegemea bahati kama Moyes anavyosema.

Usajili - Jaribio la kusajili wachezaji wakubwa dirisha kubwa la usajili lilopita lilionyesha kufeli. Baada ya hapo akamleta Marouane Fellaini (kwa £27.5m, £4m zaidi ya fedha ambayo angeweza kumsajili kabla) kuja kucheza kama kiungo mkabaji. Moyes alifanya kazi na Fellaini kwa miaka kadhaa Everton na kwa maana hiyo alikuwa akijua kabisa uwezo wa kucheza kwenye hiyo nafasi na aliamini angeweza kucheza. Hata hivyo, ameonekana hayupo ccomfortable kuicheza nafasi hiyo kwa kuangalia kiwango chake mpaka sasa - hivyo haukuwa usajili mzuri kwa United. Usajili Juan Mata umekuwa wa kuvutia, lakini ukweli unabaki kwamba Wayne Rooney anacheza kama namba 10, nafasi ambayo Mata huicheza kwa ubora, hivyo matokeo yake Mhispania huyo huchezeshwa pembeni. Mata anakosa mbio na nguvu ya kucheza kama winga asilia, hivyo Moyes anavyoendelea na mfumo wa 4-4-2 sioni mabadiliko chanya ya kupata kilicho bora kutoka Juan Mata. Akiwa tayari kashatumia kiasi cha £65.5m huku kukiwa hakuna mabadiliko yoyte yanayoonekana katika kiwango cha timu, United haipaswi kumuamini Moyes na fedha zao katika dirisha la usajili lijalo pia kutegemea yeye na wasaidizi wake kupata kilicho bora kutoka wachezaji waliopo na watakaosajiliwa.
Moyes amekuwa akivunja rekodi nzuri kwa matokeo mabaya kila kukicha. Ile hali ya timu kuiogopa Man United iliyojengwa kwa miaka mingi iliyopita imeondoka ndani ya miezi michache. Akiwa na rekodi mbovu kuliko zote dhidi ya timu za Top 6 kama kocha wa Everton, ilikuwa wazi kwamba Moyes hana uwezo wa kuiongoza United. Hali inaonekana itaendelea kuwa hivyo wakati wote Moyes atakapoendelea kuwa kocha - uongozi wake ndani ya United dhidi ya timu za Top 6 msimu huu ameambulia pointi sita tu - akiambulia sare 3 na ushindi mmoja tu. Mechi dhidi ya timu kubwa kwenye ligi ni muhimu sana - kwa pointi pia kisaikolojia. Huku United wakishindwa kuzifunga timu hizi, inaonekana wazi ni vigumu kwa United kupata mafanikio chini ya Moyes.
-shaffihdauda

JERRY TEGETE"YANGA HAUNA CHAKO RUDI SHULE AMA UHAME TEAM"

- by Unknown · - 0 Comments


BABA mzazi wa straika wa Yanga Jerry Tegete, John Tegete amemtaka mwanae achague mawili ifikapo mwisho wa msimu huu iwapo ataendelea kusugua benchi kwenye kikosi hicho.
Kocha huyo wa zamani wa Toto African ya Mwanza alisema kuwa mbali na ukocha yeye pia ni mzazi hivyo lazima afuatilie maendeleo ya mwanae.; “Naona mwanangu hana bahati na Yanga, licha ya kucheza michezo minne na kufunga mabao matano. Naamini bado anaweza kucheza na kupachika mabao, lakini kama hana nafasi basi nampa hadi mwisho wa msimu aweze kuamua kati ya kusoma au kucheza soka nje ya Yanga,” alisema.
Kama ni kurudi shule basi Jerry ni kati ya wachezaji watakaokuwa na elimu zaidi kwenye soka la Tanzania kwani tayari ni mhitimu wa kidato cha nne. Lakini amefunikwa kielimu na Reliants Lusajo mwenye Digrii ya ugavi, Salum Telela anayesoma Digrii ya Biashara na Issa Ngao naye anayesomea biashara.
SOURCE: MWANASPOTI

Monday, March 10, 2014

NAZIONA DALILI ZA KUMWACHA MKE WANGU..KWA HILI SIWEZI VUMILIA

Monday, March 10, 2014 - by Unknown · - 0 Comments




Ndugu zangu mwenzenu yamenikuta makubwa. Mimi nimeoa nikiwa mtu mzima sana. Tofauti ya umri na mke wangu ni miaka kumi na kenda. Miezi sita ya kwanza ndoa yetu ilikuwa ya furaha sana na hakika nilionja raha majinuni ya ndoa. Baada ya hapo ni mateso makubwa sana.

". Hasikii la
mwadhini wala la
mtia maji msikitini"

Mke wangu kaanzisha tabia chafu sana na isiyo mpendeza MUNGU na walimwengu pia. Ilikuwa ni mwezi wa saba wa ndoa yetu usiku wa maanani ndipo kiini cha dukuduku langu lilipoanza. Baada ya kufanya tendo la ndoa kwa raundi ya kwanza ndipo mke wangu mpendwa aliponiomba "twende chooni" akimaanisha nimwingilie kinyume na maumbile.

Kwakweli ilibidi nifanye ili kumridhisha na kumuonya kwamba iwe ni siku ile pekee. Kuanzia hapo mke wangu kaweka msimamo kuwa hanipi haki yangu mpaka nimpe "kiu yake"

Nafikiria kumpa taraka mke wangu ukizingatia bado hatujazaa.

Naombeni ushauri wana mmu wapendwa.

". Heri kufa macho
kuliko moyo"

MASKINI TAMTHILIA YA SIRI YA MTUNGI YAAMBULIA PATUPU TUZO ZA MOVIE AFRICA

- by Unknown · - 0 Comments




 
Watanzania tulifurahi kwa habari kuwa Tamthilia yetu ya Siri ya Mtungi imechaguliwa kuwania Tuzo Saba katika tuzo za Africa Magic Movie Awards 2014’ Tuzo hizo zilifanyika jumamosi hii lakini kwa Bahati Mbaya Haikuweza kupata Tuzo hata Moja...

Kinachoumiza zaidi ni hata katika kipengele ambacho ilikuwa ni lazima Siri ya Mtungi ishinde cha Best Indigenous Language Movie/Series (Swahili) kilichukuliwa na Wakenya, Njoki Muhoho – Mama Duka.

Inatia wasiwasi kidogo kwakuwa hakuna fundi wa Kiswahili duniani kumzidi mswahili mwenyewe wa Tanzania. Inapofikia hadi Mkenya anachukua kile tunachokiweza zaidi, ni ishara kuwa tunahitaji kujitafakari tunakosea wapi. Ni kweli Wakenya ni mafundi wa Kiswahili kuliko sisi? Tatizo ni nini?

“Nadhani kilichopelekea Siri ya Mtungi kukosa tuzo ni vitu viwili, kwanza tabia ya Watanzania sisi kutopenda kupiga kura, hiyo ndio tatizo la kwanza, lakini pili crew ya Siri ya Mtungi yenyewe haikuwa na nguvu kubwa kwenye kushawishi wadau katika upigaji kura. All in all jamaa wako vizuri I hope next year tutafanya vizuri. Nadhani pia waandaaji wa Tuzo zozote Tanzania wamejifunza nini maana ya Tuzo,” anasema King David, mtangazaji wa Kings FM ya Njombe.

David yupo sahihi kwa mmoja. Ni kweli kabisa, lawama ije kwetu sisi wenyewe Watanzania tulioshindwa kuwa wazalendo kwa kuwapigia kura Siri ya Mtungi washinde, lakini mfumo wa tuzo hizo ulikuwa tofauti kidogo. Kulikuwa na jumla ya vipengele 27 na ni vipengele 9 tu kati ya hivyo ndivyo vilikuwa vya watazamaji kupiga kura na kuchagua mshindi.

Kwenye vipengele vilivyokuwa vikipigiwa kura (Votable Categories) Siri ya Mtungi ilikuwa imetajwa kwenye kipengele kimoja tu ambacho ni BEST ACTOR IN A DRAMA alichokuwa ametajwa ‘Juma Rajab Rashid’ aka Cheche.

Vipengele vingine 6 ambavyo Siri ya Mtungi ilikuwa imetajwa, vilikuwa ni vile ambavyo jopo la wataalam limekaa na kuchagua mshindi linayemuona ni bora katika kipengele husika. Mara nyingi katika mfumo wa aina hii, yote yanaweza kutokea na upendeleo na mapenzi ya nchi fulani fulani yanaweza kuchukua nafasi.

Kipengele cha kupigiwa kura alichokuwa ametajwa Cheche, kilikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa Majid Michel ( Somewhere in Africa), Hlomla Dandala ( Contract), Majid Michel (House of Gold) na Tope Tedela (A Mile from Home). Ili Cheche ashinde, alitakiwa kupigiwa kura nyingi sana, na kwakweli haikuwa rahisi kuwazidi waigizaji wa Nigeria ama Afrika Kusini katika kipengele hiki japo yote yanawezekana.

Sunday, March 9, 2014

ETOO AMTHIHIRISHIA MOURINHO KUWA YEYE NI MZEE BAADA YA KUFUNGA BAO JANA

Sunday, March 9, 2014 - by Unknown · - 0 Comments




It was his first goal since Jose Mourinho was caught on camera questioning just how old the Cameroon striker even is, and Eto'o did not miss the opportunity to poke fun at the resulting controversy - his celebration saw him stagger to the corner flag bent double and holding his back, as if to suggest he is an old man....HAHA SAFI SANA KIJANA

Wednesday, February 26, 2014

KOCHA WA AL AHLY AICHAMBUA YANGA KAMA KARANGA

Wednesday, February 26, 2014 - by Unknown · - 0 Comments



Dar es Salaam. Kocha Msaidizi wa Al Ahly, Ahmed Ayoub ameichambua Yanga kwa kusema ni timu bora katika kushambulia, lakini si nzuri kwenye safu ya ulinzi.

Yanga itaivaa Al -Ahly Jumamosi hii katika pambano la raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mahojiano na mtandao wa klabu hiyo, Ayoub alisema, ushindi wa jumla ya mabao 12-2 ilioupata Yanga dhidi ya Komorozine ni uthibitisho kwamba safu yake ya ushambuliaji ni moto wa kuotea mbali.

Katika michezo 17 ya Ligi Kuu Tanzania Bara safu ya ushambuliaji wa Yanga imefunga mabao 41 na kuruhusu mabao 12 hadi sasa.

“Yanga ina safu ya ushambuliaji yenye nguvu kwani imefunga mabao 12 katika raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa ilipocheza na Komorozine ambayo matokeo ya jumla ni 12-2,” alisema Ayoub.

Aliongeza: “Ina kikosi chenye nyota watano wa kulipwa kutoka Congo,Rwanda, Burundi na Uganda ambao wana mchango mkubwa katika safu ya ushambuliaji.”

Pamoja na kusifia safu ya ushambuliaji ya Yanga, kocha Ayoub alisema atatumia udhaifu wa ngome ya ulinzi kupata matokeo mazuri.

Alisema beki ya Yanga si imara kwani haina ushirikiano wa kutosha miongoni mwa wachezaji wake husika.

“Timu ya Tanzania ina udhaifu katika eneo la ulinzi ambako kimsingi hakuna muunganiko mzuri wa wachezaji wanaocheza eneo hilo,” alisema Ayoub.

Kocha huyo alishuhudia pambano la kwanza kati ya Yanga na Komoriozine lililopigwa kwenye Uwanja wa Taifa.

Kauli ya kocha huyo ni changamoto kwa Kocha wa Yanga, Hans Van DerPluijm kwani ni wazi anatakiwa kuisuka kikamilifu ngome yake ya ulinzi kabla ya mchezo kati yake na vigogo hao wa Misri.

Safu ya ulinzi ya Yanga inaundwa na mabeki wa kati Kelvin Yondani na Nadir Haroub pamoja na mabeki wa pembeni Oscar Joshua anayecheza kushoto na Mbuyu Twite kulia.

Tuesday, February 11, 2014

YA MOYONI KUHUSU MANCHESTER UNITED..........

Tuesday, February 11, 2014 - by Unknown · - 0 Comments



Habari zenu mashibiki wote wa Man U na wadau wote wa soccer,

Awali ya yote naomba ni declare interest, mi ni die hard Man U fan, nina zaidi ya mapenzi na timu hii mi nina mahaba na timu hii. na nasukumwa na mahaba hayo kuongea haya

Ni wazi kwamba wengi wa mashabiki wa timu hii tumeipenda timu hii sio tu kwa sababu ilikua inafundishwa na SAF bali ni kwa sababu ilikua ni timu ya washindi, timu yenekuleta ushindani mpaka dakika ya mwisho, how many times tumechomoa magoli dk za 90,94 au 96 wakati wapinzania washaamini ushindi upo kwao it was in our DNA, that is Manchester I used to know, je Man U hiyo imeenda wapi…?
Naelewa na kuamini msemo usemao mvumilivu ula mbivu lakini vilevile dalili ya mvua ni mawingu na chelewa chelewa utakuta mwana sio wako.
Wapo wadu wanajaribu kusema hii hali ya timu yetu sa hivi ni kawaida tu hata SAF aliipitia, katika swala la kuipitia sina ubishi nalo ila kusema ni kawaida hapo ndio tunatofautiana,
Hivi expectation za Man u wakati Fergie anakabidhiwa timu zilikua sawa na za Man U ya sasa…? Aliikuta timu hipo katika level gani katika timu za Uingereza…? Hivi expectations walizonazo washabiki wa Swansea kwa kocha wao mpya ni sawa na za mashabiki wa Man U…? je mnataka kusema lengo la kuleta kocha mpya ilikua ni kutoka level zetu za big 4 kwenda kuwa wafalme wa big 7…?
Mpaka hapo nimeshaonesha mlengo wangu ni hupi, YES simkubali Moyes na I put all blames on him kwa kiwango kibaya cha timu yetu cha kihistoria, wanao msupport Daudi wamekua wakisema tumpe muda anajenga timu, nafikiri wangesema tumpe muda maana anabomoa iliyokuwepo kwanza ndio baadae aje kujenge timu mpya….
Timu hii iliyoonekana mbovu leo hii ndio timu hiyo hiyo iliyochokua vikombe msimu uliopita under SAF na benchi lake la ufundi, cha kustaajabisha daudi alipokuja akataka kuonesha ulimwengu ye ni mjuzi wa mambo akafukuza bench lote la ufundi nakuleta lake amabao limeprove failure, binafsi nilifikiri Moyes angekua na short term plan na long term plan, short term plan ingekua ni kuimantain hadhi ya Man U kwa kupitia timu hii hii aliyokuta nahilii ingewezekana kwa kuliacha bench la ufundi alilolikuta maana ndio linaimudu hii timu while long term plan ingekua kutengeneza timu yake mweneyewe kwa kufanya mabadiliko kidogo kidogo amabayo hayata athili timu yote, matokeo yake katuletea wakina Philip Nevell….kweli of all legends wa man U huyu dogo ndio ameona awe mshauri wake…
Na ikumbukwe Moyes ni Manager na sio coacher/mkufunzi na kazi ya manager sio kumfundisha RVP kufunga au Vidic kukaba bali ni kuleta game plan afu wachezaji wanaifollow hiyo game plan, na ili kuwafanya wachezaji wamaiweze game plan yako kwanza ni mpka wae na imani na wewe, pili hiyo game plan yako hiwe workable na mwisho kabisa laziama uwe the good MOTIVATOR, na manager mazuri dunianiani ni good motivator hata kama timu inamapungufu as long as kocha wao yupo wataperform tu kwa kiwango sawa na timu zilizo bora, Moyes kashindwa kabisa hii…. Mbinu za man U siku hizi the are very obvious and predectable mpaka timu zinazaotaka shuka daraja can crack our plans easily and use them against us, mfano game ya juzi na Fulham, mbinu za moyes zilikua old school kabisa, tanua uwanja then piga long crosses, by the way tulipiga cross zaidi ya 80 and then what…!! I wonder mata alinunuliwa kwa ajili gani kama hii ndio game plan ya Moyes
“Moyes the chosen one” hii kauli ndio inatuua sasa man u, sijui ni nini SAF alikiona kwa Moyes mpaka akaamini is the right guy for the Job, na sijui alishindanishwa na nani na kuibuka kinara au kipi exactly walikiona kwa Moyes, binafsi nilipoona The Boss kampendekeza sikua na shaka kabisa ni kiaamini thr Boss siku zote huwa yuko sawa kwenye maaamuzi yake, ila sas nahisi na naaamini on this he gotta it all wrong, ikumbukwe huyo Fergie before coming to Man he was already the winner, he had already won the Scottish League with Aberdeen and he kills the domination of Rangers and Celtics akaja England akaikuta man U hiko dhoofu bin hali, lakini akawatoa waflme Liverpool kileleni, Moyes c.v yake inaonesha alishawai kushinda nini au nini kilichomfanya apewe timu kubwa kiasi hiki…?
Hivi tumekua West Ham united kwamba tunamantain kubakia kwenye league tu….timu imekosa ushindani kabisa afu watu tuansema apewe muda, sa apewe muda wa nini….
MWISHO; nothing personal, ila Moyes kaishaprove he gotta nothing to offer for Man U tukubali tu tulibugi hapo, na ka nakosa Moyes prove me wrong leta ushindi nyumbani, ntakuja hapa na kusema YES you are the right person for our team after all hakuna shabiki anafurahia kushindwa wala hakuna shabiki anajinyonga au kumchoma mtu kisu timu yake inaposhinda kwa kuwa hatupati ushindi as we used to get basi something is wrong somewhere, and it is my duty as a fan to shout about it
By Mbeky From JF

Sunday, December 15, 2013

TEAM YA GOR MAHIA YAPATA PIGO WACHEZAJI VINARA AKIWEMO IVO MAPUNDA WAONDOKA

Sunday, December 15, 2013 - by Unknown · - 0 Comments




WAMEIBOMOA Gor Mahia. Ndivyo unavyoweza kusema kuhusiana na hatua ya Simba ya Tanzania kuwasajili kipa, Ivo Mapunda na beki Donaldi Musoti.

Klabu hiyo ya Tanzania ambayo maofisa wake walikuwapo jijini Nairobi wakati wa mashindano ya Cecafa Senior Challenge Cup yaliyomalizika juzi Alhamisi, walikamilisha usajili wa wawili hao jana Ijumaa.

Mapunda aling’ara katika michuano hiyo akiwa na timu ya Tanzania Bara, wakati Musoti alikuwa katika kikosi cha Kenya. Mapunda amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu wakati Musoti amesaini miaka miwili.

Musoti alisema: “Nimefurahi sana kusaini Simba, nakwenda kufanya kazi na Loga (Zdravko Logarusic) ambaye nimekaa naye Gor Mahia kwa mafanikio.

“Nina uzoefu wa kutosha na soka la Afrika Mashariki na ninadhani nitafanya kazi nzuri na Simba kama Wakenya wenzangu waliopita, kikubwa ni ushirikiano tu.”

Katika kikosi cha Gor Mahia,Musoti hucheza sambamba na Ivan Anguyo au Edwin Lavatsa.

Makamu Mwenyekiti wa Kwanza wa Gor Mahia, Faz Ochieng, amekiri kuwa kuondoka kwa wawili hao ni pigo kwao na watakaa kujadiliana nini cha kufanya.

“Sijapata taarifa rasmi za kuondoka kwao, lakini mikataba yao inamalizika mwezi huu na ilikuwa tukae nao kujadiliana juu ya mikataba mipya,” alisema.

Gor Mahia itakuwa imepata pigo kubwa baada ya wachezaji hao kusaini Simba kwani walikuwa tegemeo kwao na waliibeba kwenye Ligi Kuu Kenya msimu uliomalizika ambapo timu hiyo ilitwaa ubingwa.

Mapema wiki hii matajiri wa Gor Mahia walijinadi kuwa watahakikisha kwa gharama yoyote ile wanawabakiza wachezaji hao jambo ambalo limegonga mwamba kwani viongozi wa Simba waliowasili usiku wa Jumanne iliyopita wameshamaliza kazi.

Kuthibitisha jinsi klabu hiyo ilivyopata pigo, baadhi ya mashabiki wa Gor Mahia jana Ijumaa walivamia ofisi za timu hiyo zilizopo maeneo ya uwanja wa soka wa Nyayo wakiwa na mavuvuzela na kuwapigia kelele viongozi wao wakiwahoji imekuwaje wamewaachia wawili hao kujiunga na Simba.

Mashabiki hao waliokuwa zaidi ya 50 wamechukizwa na jambo hilo na kuwaoana viongozi wao ni wazembe kwani klabu hiyo ni kubwana ina fedha za kuwabakiza

Tuesday, December 10, 2013

KILI STARS YAONDOLEWA CHALENJI, YAPIGWA NA HARAMBEE STARS 1-0

Tuesday, December 10, 2013 - by Unknown · - 0 Comments


TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' imeondolewa kwenye michuano ya Kombe la Chalenji inayoendelea nchini Kenya baada ya kufungwa na timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars' bao1-0 katika mechi iliyomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Nyayo uliopo jijini Nairob

Saturday, November 30, 2013

TANZANIA YAPANDA KIWANGO CHA SOKA KATIKA VIWANGO VYA FIFA

Saturday, November 30, 2013 - by Unknown · - 0 Comments




Tanzania imepanda nafasi tano zaidi katika viwango vya Fifa, hivyo sasa kuwa ya 124, huku Zimbabwe ambayo ilitoka sare tasa na Taifa Stars katika mechi ya kirafiki iliyopigwa Uwanja wa Taifa mwezi huu, ikishuka kwa nafasi nne na sasa kuwa ya 106.

Zambia ambayo jana ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Kilimanjaro Stars ikiwa kama timu alikwa kwenye michuano ya Kombe la Chalenji iliyoanza juzi jijini Nairobi, Kenya, imeshuka nafasi tano na sasa ni ya 72 katika viwango hivyo.

Katika nchi za Ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Uganda ndiyo inayoshika nafasi ya juu ikiwa ya 86 duniani licha ya kushuka kwa nafasi moja mwezi huu.

Burundi ambayo imepanda kwa nafasi tisa, inashika nafasi ya pili kwa upande wa Cecafa ikiwa nafasi ya 112 duniani, ikifuatiwa na Kenya iliyopanda kwa nafasi moja na kuwa ya 117 duniani, huku Rwanda iliyopanda kwa nafasi mbili na kuwa ya 127, ikiburuza mkia kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Jirani zetu DR Congo wanashika nafasi ya 84 baada ya kupanda kwa nafasi saba zaidi mwezi huu, huku kwa upande wa Afrika Ivory Coast ikiongoza na kwa dunia ikishika nafasi ya 17.

Ghana iliyoshuka kwa nafasi moja, inashika nafasi ya pili kwa Afrika huku kwa dunia ikiwa ya 24 na kwa bara hili ikifuatiwa na Algeria iliyopo nafasi ya 26 duniani baada ya kupanda nafasi sita. 

Hispania ndiyo kinara katika vingo hivyo ikifuatiwa na Ujerumani, Argentina, Colombia, Ureno, Uruguay, Italia, Switzerland , Uholanzi, Brazil, Ubelgiji, Ugiriki na England ikiwa ya 13 baada ya kushuka kwa nafasi tatu mwezi huu.

Thursday, November 21, 2013

IVO MAPUNDA : JUMA KASEJA BADO NI KIPA BORA TANZANIA

Thursday, November 21, 2013 - by Unknown · - 0 Comments




Kipa wa Taifa Stars na Gor Mahia, Ivo Mapunda amemtoa wasiwasi mwenzake Juma Kaseja kwa kumwambia ‘wewe bado ni Tanzania one’.
Mapunda alisema uamuzi wa Kaseja kwenda Yanga ni sahihi na kumtaka atulize akili ikiwezekana atafute watu wa saikolojia kwa ajili ya kumpa ushauri.
“Kaseja ni kipa bora, wanaosema ameshuka kiwango nawashangaa watakuwa hawajui vizuri soka,”alisema Mapunda.
Alisema,”Yanga wamelamba dume, atawasaidia, mimi binafsi namkubali, yupo kwenye kiwango kizuri, ana uzoefu wa muda mrefu Simba watajutia kumuacha.”
“Mimi namuomba Kaseja atulize akili, mimi mbona walisema nimekwisha sina jipya, lakini mbona nipo kwenye fomu nina uwezo wa kucheza hata miaka 10 mbele, kikubwa ni nidhamu ya mazoezi na kujitunza,”alisema Mapunda.
Kauli ya Ivo imekuja baada ya Kaseja kumwaga wino wa kuichezea Yanga kwa kitita cha sh 40 milioni baada ya kukaa nje kwa muda. Kaseja alisajiliwa Simba mwaka 2003 akitoka Moro United na tangu wakati huo alikuwa kipa tegemeo wa Simba kwa misimu tisa ingawa kwa msimu mmoja wa 2008/2009 aliichezea Yanga kabla ya kurudi tena Simba.

Tuesday, November 19, 2013

ADEN RAGE ASIMAMISHWA NA KAMATI YA UTENDAJI YA SIMBA

Tuesday, November 19, 2013 - by Unknown · - 0 Comments




Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba iliyokutana jana usiku, imemsimamisha kazi Mwenyekiti Ismail Aden Rage.
Rage amesimamishwa kazi kutokana na masuala kadhaa ya kiutendaji , lakini kubwa imeelezwa ni suala la mauzo ya mchezaji Emmanuel Okwi.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI