Wednesday, September 11, 2013

ALICHOSEMA RASHID MATUMLA KUHUSU MDOGO WAKE KUKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA



Bondia Rashid ‘Snake man’ Matumla amedai endapo itathibitika mdogo wake Mkwanda anajihusisha kusafirisha dawa za kulevya atakuwa ameipa fedheha familia yao.
“Mkwanda ameipa fedhea familia yetu, hii ni aibu kubwa ukizingatia vitendo hivyo vinakatazwa si Tanzania tu bali na kwenye nchi nyingine”
Mkwanda ambaye kwa mujibu wa Rashid alipumzika kucheza ngumi miaka kadhaa iliyopita kutokana na kusumbuliwa na maradhi alikamatwa wiki iliyopita nchini Ethiopia akiwa na mchezaji wa zamani wa Simba, Joseph Kaniki na leo watapandishwa kizimbani nchini humo kwa tuhuma hiyo.
“Mimi mwenyewe nashangaa ni lini amejiingiza kwenye kazi hiyo, hata wakati anaondoka hakuniaga, mimi kaka yao na familia hatuelewi chochote,” alisema Matumla.
Alisema mdogo wake huyo alikuwa amebadilisha uraia na kuchukua uraia wa Sweden na kuoa hukohuko Sweden licha ya kwamba hapa Tanzania alikuwa amepanga Mbagala, Dar es Salaam na alikuwa anakuja na kukaa kwa muda na kisha kuondoka.
“Ni mwezi sasa umepita sina taarifa naye na hata wakati anaondoka hakuniaga, nimesikia kupitia vyombo vya habari kitendo cha mdogo wangu kukamatwa kimenisikitisha mno, siyo siri nimekwazika na ninarudia kusema hii ni fedheha kwenye familia yetu,” alisema bingwa huyo wa zamani wa dunia wa WBU. Rekodi zinaonyesha kabla ya kupumzika kwa muda kucheza ngumi, Mkwanda alishinda mapambano manane (sita kwa KO) alipigwa mara tatu zote kwa KO alitoka sare mara moja tangu 2004.
Ripoti hii imeandaliwa na gazeti la Mwananchi

Tags:

0 Responses to “ALICHOSEMA RASHID MATUMLA KUHUSU MDOGO WAKE KUKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI