Saturday, March 29, 2014
Wajumbe hao walitangaza uamuzi huo bungeni kutokana na makubaliano yaliyofikiwa katika kamati ndogo ya maridhiano iliyofanyika jana asubuhi baada ya kushindwa kuafikiana katika kikao cha awali kilichofanyika juzi kuanzia saa 3:00 usiku hadi usiku wa manane ili kunusuru kukwama kwa Bunge hilo.
Kabla ya uamuzi huo, Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta alisema juzi usiku walikutana hadi usiku wa manane baada ya hapo, walikabidhi kamati ndogo yenye mchanganyiko wa wajumbe kutoka Kamati ya Kanuni na Kamati ya Maridhiano.
“Baada ya kukamilisha kazi, wajumbe wa kamati ndogo watatoa taarifa hapa ambao ni John Mnyika, Profesa Ibrahimu Lipumba, Vual Ali Vual na Askofu Donald Mtetemela,”alisema Sitta.
Akitoa taarifa ya maridhiano hayo, kwa niaba Freeman Mbowe, Mjumbe John Mnyika alisema, alianza kwa kunukuu kitabu kilichoandikwa na Mwalimu Nyerere, mwaka 1962 chenye ujumbe mahususi kwa Chama cha TANU akisema ujumbe huo kwa sasa ni sahihi kwa watu wengi na taasisi ikiwamo CCM.
Mnyika pia alisema Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) hawana nia yoyote ya kuvuruga mchakato wa katiba kama ambavyo imeelezwa katika siku za karibuni na viongozi, kwani wazo la kutaka Katiba Mpya imekuwa ni kilio chao cha muda mrefu.
Naye Profesa Lipumba alisema suala ambalo tumekuwa tukisimamia kwa muda mrefu suala ambalo lina utata, kati ambao wanapenda kura za uwazi na wale wa siri.
Alisema: “Tuliletewa mchanganyiko wa uwazi na siri, lakini maana yake ni kura ya uwazi, wenzetu wamekuwa na msimamo mkali hata hili la kufanya uamuzi ilikuwa tufanye kwa siri, lakini hata hivyo hawakukubali.”
“Tulifanya uamuzi ili tusonge mbele, basi tulipendekeza upigaji kura wa kuamua tupige kura kwa mfumo wa siri, lakini pia wenzetu walikataa,”alisema Profesa Lipumba.
Alisema kwa kuzingatia kutokwama kwa zoezi la kuanza kujadili rasimu, wameamua kukubali kutokubaliana.
“Ili kusonga mbele tunahitaji kusonga mbele tuanze kujadili Katiba, natoa wito kwa wenzangu wa chama tawala kwa kuwa mpo wengi mnadhamana kubwa, ni vyema mkawa na utaratibu wa kuwasikiliza wachache,” alisema.
Mjumbe Vuai Ali Vuai alisema, wamefikia maridhiano hayo, ili kuwezesha kuendelea na mchakato wa katiba mpya kwani kila upande uliendelea kutetea msimamo wake hata katika kikao cha maridhiano.
Friday, March 28, 2014
"Wanaotetea kura ya siri itumike katika kupitisha Katiba ya Watanzania, wanaunga mkono sera za ushoga, ni wale ambao vyama vyao vinazaminiwa na wanaotetea sera za ushioga," alisema Nchemba bungeni.
Kutokana na Kauli ya Nchemba, bunge hilo lilipuka likitaka aombe radhi huku akionyesha kusita kuomba radhi, lakini Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan alimtaka aombe radhi mara kadhaa.
"Mheshimiwa Mwigulu, naomba usimame na kuomba radhi wabunge wenzako, tafadhali simama," alisema Samia
Baada ya kauli ya Makamu Mwenyekiti Samia, Mwigulu alisimama na kusema: "Mheshimwa Makamu Mwenyekiti, Naomba radhi kwa wote wanaodhani wao wako hivyo kama nilivyosema."
Kauli hiyo ilionekana kuendelea kuwachefua wabunge wa bunge hilo huku wakimzomea na kumtaka aombe radhi kwa kuwa bado alikuwa hajaomba radhi moja kwa moja bali kauli yake ilionekana kuwa na utata.
Kwa mara nyingine, Makamu Mwenyekiti, Samia alisimama tena na kumtaka aombe radhi. "Mheshimiwa Mwigulu tafadhali omba radhi bila condition, tafadhali, bila kuomba radhi, Bunge haliwezi kuendela, na ninyi wabunge wengine kaeni kimya bila utulivu hatuwezi kusikilizana, tafadhali," alisema Samia.
Baada ya kauli kauli ya Makamu Mwenyekiti, Samia, Mwigulu alisimama tena na kuomba radhi kwa heshima na bunge kuendelea na utaratibu wake.
"Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti, nakiheshimu hicho kiti hapo mbele, siwezi kudharau, Naomba radhi kwa wote nilowaudhi," alisema Mwigukulu na kukaa chini.
Baada ya kauli ya Mwigulu ya kuomba radhi, shughuli za bunge ziliendelea kama kawaida
Alipokuwa spika wa bunge la 9,alitupa mwamko wa kufuatilia vikao vya bunge.Hasa pale aliporuhusu uundwaji wa kamati ya Mwakyembe iliyochunguza dili la richmond na hatimaye kupelekea kumwagika kwa unga wa EL.Wengi tulijua kuwa mzee amedhamilia kuleta mapinduzi ya kisiasa,kwamba hajali ni mtu wa chama gani,ila anachojali ni viwango na kasi.
Juzi ameaminika na kuchaguliwa kwa kishindo pale bungeni ili kuongoza bunge la katiba,akarudia katika maelezo yake kuwa atakuwa yule yule wa viwango na kasi,wengi wakampigia vigelegele,hata mimi nilifurahi na kurukaruka nikijua jembe limerudi shambani.
Ghafla,akatuacha solemba,akatuduwaza na kutuacha na mshangao mkubwa.Hii ilikuwa ni wiki jana pale alipokubali kanuni zisivunjwe ila zipindishwe.Ilikua amkaribishe JK aanze kuzindua bunge kisha afuatiwe na Warioba.Yeye 6,akapiga tiktaka akiwa amevaa taulo,akamleta kwanza Warioba ! Hii haikuwa kwa bahati mbaya,ila ilikuwa planned kabsaa! Yakawa yaliyokuwa na wote tumeshuhudia na kuhudhunika.Hivi kanuni walizojitungia zitafuatwa kweli kama wa kwanza kuzivunja ni 6 na rais wa nchi!?
Wadukuzi wa siasa zetu wanasema 6 alipewa shinikizo na chama chake ili aruhusu kwanza mwenyemeza wao(mwenyekiti) atanguliwe na Mzee Warioba ili baadae mwenyekiti aje kujibu mapigo.Vipi kama angetangulia mwenyekiti na kisha Warioba angefuata,je,mwenyekiti angesomeka kwa ile hotuba yake kweli?
Kwanini 6 anaonekana kuwa refa anayebeba timu fulani waziwazi? Mmeona kwenye kamati za uongozi alivyoteua?
Je, 6 amechuja au amepauka ?
Ukawa inayoongozwa na vinara wa vyama vikubwa vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi pamoja na vingine vidogo visivyokuwa na wabunge, inaonekana kuwa mwiba kwa Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta kwa kudhibiti uvunjwaji wa kanuni ili kuibeba CCM.
Awali CCM ililipuuza kundi hilo na kulibeza, lakini baada ya kuona nguvu yake wakati wa kumtetea Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba apewe muda wa kutosha, hofu ilitanda.
Thursday, March 27, 2014
Katika tuhuma hizo, Wenje alimtaja Waziri Profesa Jumanne Maghembe, Dk. Shukuru Kawambwa na Gaudensia Kabaka akisema kuwa walitoa rushwa ya vyakula, maji na vinywaji kwa wajumbe hao ili waunge mkono msimamo wa serikali mbili.
Kauli hiyo, iliyotolewa katika mjadala wa mabadiliko ya kanuni, ilisababisha mawaziri hao kunyanyuka kujibu tuhuma hizo, huku Wenje akisisitiza kuwa aliyoyasema ni kweli tupu.
Vilevile baadhi ya wajumbe wanaotoka katika kundi hilo walicharuka na kujaribu kujitetea huku mmojawapo akitishia kuwa iwapo Wenje asingeomba radhi, asingetoka ndani ya Bunge hilo.
Hoja ilipoanzia
Wenje, ambaye pia ni mbunge wa Nyamagana (Chadema), alianza kwa kueleza kwamba wapinzani “walilia” sana kuwa Bunge la Katiba lisingekuwa na usawa kutokana na Chama cha Mapinduzi kuwa na wajumbe wengi, ndipo ikaonekana wapatikane wajumbe wengine 201, lakini jambo la ajabu ni kwamba walioteuliwa katika kundi hilo asilimia 80 ni makada wa CCM akiwamo mzee maarufu ambaye ameingizwa kama mganga wa jadi.
Ingawa hakumtaja jina, Wenje alikuwa anamaanisha kada mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale-Mwiru aliyeteuliwa kupitia kundi la waganga wa jadi.
Kuhusu rushwa, Wenje alisema:“…Sasa kuna wajumbe wa kundi la 201 walipelekwa kwa Profesa Maghembe na Dk. Kawambwa wamepeana rushwa, vikao vingi vilifanyika usiku. Hii haikubaliki.”
Baada ya kauli hiyo ya Wenje, Profesa Maghembe alisimama ghafla huku akionekana kutaharuki, ambapo Makamu Mwenyekiti Samia Suluhu Hassan alimpa nafasi ya kujieleza.
Profesa Maghembe alikiri kuwakaribisha baadhi ya wajumbe wa kundi hilo, akieleza kwamba ilikuwa ni katika hali ya ukarimu uliozoeleka miongoni mwa jamii ya Kitanzania.
“Kuna kundi lipo hapa ambalo linafanya kazi ya kudhalilisha wenzao. Ni kweli niliwaalika kwa chakula wajumbe hao kwa taratibu za kawaida, lakini hakuna mbunge hapa anayeshindwa kujinunulia chakula, hakuna anayeweza kupewa rushwa.
“Kwa sababu hiyo ninaomba kiti chako kimtake mjumbe aliyewasilisha hoja hiyo aniombe radhi. Wenje aniombe radhi,” alisema Profesa Maghembe akiwa katika hali ya hasira, huku kukiwa na sauti za kuzomea na kushangilia kutoka kwa wajumbe.
Makamu mwenyekiti pia alifanya jitihada za kuwataka wajumbe kuwa wavumilivu, huku akitoa nafasi kwa Dk. Kawambwa kujieleza akisisitiza kwamba ni tuhuma nzito.
Kawambwa alisema: “Ni kweli nilikutana nao; ni wajumbe ambao wanatoka kwenye taasisi zinazojihusisha na masuala ya elimu, lakini mbona wameshafanya mikutano yao mingine mingi ambayo mimi hawakuniita. Kama mtu akiwa hana hoja bora akae chini.”
Makamu Mwenyekiti alimtaka Wenje aombe radhi kutokana na kauli yake, lakini katika hali ya kushangaza mjumbe huyo alisisitiza kwamba Profesa Maghembe na Dk. Kawambwa wamekiri.
“Maghembe amekiri aliwaita wafugaji na wavuvi ndiyo waliokula chakula cha rushwa, pia wapo wengine walienda kwa Waziri Gaudensia Kabaka, kuna ushahidi mama mmoja siwezi kumtaja jina hapa alikwenda huko akafukuzwa, nitakupa jina lake mwenyekiti baadaye. Aliambiwa kwamba anatoa siri… hoja iliyojadiliwa huko ilikuwa ni kwamba msimamo ni wa serikali mbili… rushwa ya chakula, maji na bahasha walipewa,” alisema Wenje na kusababisha kulipuka kwa kelele zaidi.
Wenje aliongeza kuwa kuna wajumbe wengine walikwenda hadi kwa waziri mkuu ambako walikula, walikunywa hadi saa 7:00 usiku.
Alisema wengine walikwenda kwa Gaudensia Kabaka (Waziri wa Kazi na Ajira) na walikula na kunywa na kupewa bahasha.
Baada ya Wenje kukaa, baadhi ya wajumbe wa kundi la 201 walichachamaa wakitaka kutetea hadhi yao, akiwamo mjumbe kutoka kundi la wafugaji, Esther Juma aliyesema hawatendewi haki kama kundi kusema kwamba walihongwa.
Alisema yeye ana ng’ombe 3,000 na asingeweza kwenda kupokea rushwa ya chakula na kumtaka mbunge huyo kuwaomba radhi la sivyo asingetoka mlangoni.
Wakati mjadala huo ukiendelea, mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta aliyekuwa ametoka kwa udhuru, alirejea kimya kimya, na kumtaka Wenje kueleza iwapo anadhani kauli yake haikuwaudhi baadhi ya wajumbe.
Wenje alikiri kuwa ni kweli baadhi ya wajumbe wameudhika kutokana na ukweli aliosema dhidi yao na kuwaomba radhi kwa ukweli huo.
Kauli hiyo ilimfanya Sitta kutangaza kuwa anapeleka suala hilo kwenye Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge na uamuzi utakaotolewa atautangaza bungeni.
Kuna njama. Maneno haya mawili ndiyo yametumiwa na pande mbili zinazopingana ndani ya Bunge Maalumu la Katiba, kuelezea hali iliyojitokeza jana wakati wa kikao cha Bunge hilo kuhusu mvutano wa mabadiliko ya kanuni.
Njama zinazoelezwa na pande hizo ni za kuvuruga mchakato wa Katiba Mpya, zikirejea yaliyotokea jana jioni ikiwamo zomeazomea hali iliyomlazimu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta kuliahirisha Bunge hadi leo jioni.
Baada ya kuahirisha Bunge hilo, Sitta alikutana na waandishi wa habari na kusema kwamba kuna njama za baadhi ya wanasiasa kutumia vurugu kuhujumu mchakato wa upatikanaji wa Katiba, badala ya kujenga hoja.
Bila kuwataja wanasiasa hao, Sitta alisema ikiwa hawataki kuendelea na mchakato huo, basi waondoke na kuwaacha wenye nia njema.
“Wanasiasa hawa wamedhamiria kuvuruga mchakato wa Katiba, tuhuma ambazo tumetuhumiwa leo na Lissu (Tundu) ni uongo na uzushi, mimi sihusiki na kupeleka marekebisho ya kanuni kwenye Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge,” alisema Sitta.
Sitta alikuwa anajibu mchango wa mjumbe wa Bunge, Tundu Lissu alioutoa mapema kwenye kikao cha jioni, akipinga kilichoelezwa ni njama za kutaka kubadili kanuni kinyemela ili kumsaidia mwenyekiti kulidhibiti Bunge.
Sitta alisema kwa kuzingatia kanuni ya 59 (1), Kamati ya Uongozi ina mamlaka ya kupeleka marekebisho ya kanuni ili kuliwezesha Bunge kufanya kazi vizuri.
Alisema hoja kwamba haiwezekani kufanyika mabadiliko hata kabla ya kuanza kutumika kanuni, siyo ya msingi kwani kila kitu kinabadilika kutokana na mazingira yake.
“Kamati ya Uongozi ndiyo ilipeleka waraka wa mabadiliko ya kanuni kwa Kamati ya Kanuni na Haki kwa kuzingatia kanuni, lakini hata kabla ya kujadiliwa na kamati husika inaonekana kuna wajumbe ndiyo wameichukua na kuifikisha bungeni,” alisema Sitta.
Alisema kwa kiasi kikubwa marekebisho ambayo yangesomwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Pandu Ameir Kificho, yalilenga kutoa ufumbuzi wa kanuni ya 37 na 38 juu ya upigaji kura ama uwe wa wazi au siri.
Sitta alisema pamoja na hilo, kulikuwa na marekebisho ya msingi kama kuweka utaratibu mzuri wa majadiliano katika kamati pia kuweka utaratibu wa vikao vya Bunge kuanzia Jumatatu hadi Jumapili.
“Mengi ambayo alikuwa anayasema Lissu kama ni takataka hayakuwapo katika taarifa ya Kificho,” alisema Sitta.
Wednesday, March 26, 2014
Akihojiwa na Sauti ya Ujerumani Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti wa UKAWA amekiri kwamba ni kweli mpango wa kujitoa upo na kwamba wamekubaliana kuvumilia kwa muda kuwapa Ccm muda wa kufikiria mara mbili kuaha kuvuruga mchakato. "Ni kweli wazo la kujitoa lilikuwepo tangu jana na katika kikao cha leo, lakini tumesihi wenzetu kuvumila kidogo huku tukiwapa nafasi wenzetu kujaribu kerekebisha hali inyoendelea."
Amesma pia kwamba UKAWA hawalalamikii nafasi katika kamatia bali uvunjifu wa makusudi wa kanuni.
Monday, March 24, 2014
Kwa neno moja unaweza kusema kwamba wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba na wananchi kwa ujumla wako “njiapanda”.
Hii ni baada ya hotuba ya ufunguzi wa Bunge hilo iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete kuibua mambo mazito ambayo kimsingi yanatofautiana na mapendekezo yaliyomo katika Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa bungeni na mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Huku wananchi wakijiuliza nini hatima ya Bunge hilo baada ya hotuba hiyo, baadhi ya wajumbe ambao wiki hii ndiyo wanaanza kujadili rasimu hiyo, watakuwa katika wakati mgumu wa kuamua wafuate maoni ya nani, kati ya viongozi hao wawili.
Ingawa Rais Kikwete amesema mara kadhaa kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba ndiyo waamuzi. Mambo mengi aliyoibua yanaonyesha kutokubaliana kwake na baadhi ya maoni ya wananchi yaliyomo katika rasimu, ambayo Jaji Warioba amewahi kusema kuwa yanatakiwa kuheshimiwa.
Wakizungumzia tofauti hizo, mjumbe wa Bunge la Katiba, Ezekiah Oluoch alisema kauli za Rais Kikwete na Jaji Warioba zimezidi kuwagawa wajumbe wa Bunge hilo kwa maelezo kuwa tangu awali wajumbe hao walikuwa wamegawanyika katika makundi mawili; ya wanaotaka muundo wa Muungano uwe wa serikali tatu na wale wanaotaka serikali mbili.
Alisema kama suala la muundo wa Serikali likishindikana kupatiwa mwafaka ni vyema likarudishwa kwa wananchi ili wapige kura ya maoni kuchagua aina wanayoitaka, kisha suala hilo lirejeshwe tena katika Bunge la Katiba kwa ajili ya kuboreshwa.
“Rais alipoanza kuzungumza alikuwa kama mkuu wa nchi lakini mwisho wa hotuba yake aligeuka kuwa mwenyekiti wa CCM. Kifupi alichokizungumza kimekwenda tofauti na wadhifa wake,” alisema.
Naye Deo Filikunjombe alisema: “Nadhani kwa hotuba hizi mbili, kazi ya wajumbe wa Bunge la Katiba itakuwa rahisi. Maana sasa wameshajua uzuri na ubaya wa serikali tatu na mbili.
“Hata kama kutakuwa na tofauti, wananchi ndiyo watakuwa wa mwisho kuamua kama Katiba hii ipite au isipite. Tunachotakiwa wajumbe ni kuwa makini na uamuzi wetu.”
Naye Yusuf Manyanga alisema: “Bunge la Katiba limejaa watu wenye busara. Sidhani kama tutashindwa kuelewana maana hata katika biashara ya utumbo inzi ni wengi lakini utumbo unauzika.”
Katika hotuba yake aliyoitoa Ijumaa iliyopita Rais Kikwete aligusia mambo saba ya msingi yaliyomo katika rasimu ya Katiba na kutaka yatazamwe kwa kina, huku akibainisha kuwa mengine hayawezekani kutekelezeka.
Katiba tunaotoka makundi mbalimbali na pia tunaoamini katika kauli mbiu isemayo “TANZANIA KWANZA”, tunapenda kutoa tamko rasmi la kuunga mkono hotuba aliyoitoa Mheshimiwa Rais alipokuwa akihutubia Bunge Maalum la Katiba Tarehe 20/03/2014 kama ifuatavyo:
Kwanza, tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kwa hotuba yake aliyoitoa wakati akizundua Bunge Maalum la Katiba tarehe 20 Machi 2014.
Tunaamini Rais, kama Mkuu wa Nchi, alikuwa na haki na wajibu wa kutoa mwelekeo na maono yake kuhusu Rasimu ya Katiba na hatua hii tuliyonayo sasa ya kuipitia Rasimu kwenye Bunge la Katiba.
Tunafarijika kwamba hotuba hiyo imepokelewa vizuri na Watanzania wengi kwenye kila kona ya nchi yetu na wengi wao wamekuwa wakitutumia ujumbe wakituhimiza kuizingatia hotuba hiyo katika kutimiza wajibu wetu.
Pili, tunamshukuru Rais kwa uchambuzi wake wa kina wa Rasimu na ushauri wake kwetu kuhusu haja ya kuweka taifa mbele, kushawishiana kwa hoja kuliko kulazimisha hoja na haja ya kutunga Katiba itakayoliimarisha taifa letu na kuendeleza umoja na ustawi wa
Watanzania. Sisi wana TANZANIA
KWANZA tutaendelea kushawishi kwa hoja na wala hatutalazimisha.
Tatu, tumeshangazwa na hamaki
iliyoonyeshwa na baadhi ya wajumbe wenzetu kuhusu hotuba ya Rais.
Tunasikitishwa na kauli zao zenye
mwelekeo wa kuhujumu mchakato wa kupata Katiba mpya. Viongozi
hawahawa wanaotoa kauli hizi
walionekana wakishangilia hotuba ya Rais pale aliposema yale waliyokuwa wanakubaliana nayo. Iweje watishie vurugu na kususia kisa tu Rais kasema baadhi ya mambo wasiyokubaliana nayo.
Ustahamilivu wa kidemokrasia,
ustaarabu na hekima ya uongozi na utu uzima hautaki hivyo.Hotuba ya Rais imeweka wazi faida na hasara za mifumo yote ya Muungano wa Nchi yetu kwa hoja ili Watanzania wawe na fursa pana zaidi ya kutafakari na mwisho kuamua.
Mheshimiwa Rais ametimiza kauli yake ya kushawishi kwa hoja na si kwa kulazimisha.
Nne, Hotuba ya Mheshimiwa Rais
haikuvuruga wala kuingilia mchakato uliopo mbele yetu. Rais hakuingilia kanuni za Bunge maalum
tulizozipitisha, Rais hakubadilisha
Sheria ya mabadiliko ya Katiba, Rais
hakupiga kura kwenye vifungu vya
Katiba, Rais ameanza kwa kuipongeza Tume ya Mh. Jaji Warioba na kuipongeza kuwasilishaji wake.
Alichokifanya Mheshimiwa Rais kama kiongozi mkuu wa Nchi mwenye hekima na busara na uchungu wa Nchi yake na kutambua dhamana aliyopewa na Watanzania wote bila kujali makundi ameelezea faida na hasara za mifumo ya Serikali iliyowasilishwa kwenye hotuba ya Mheshimiwa Mwenyekiti wa Tume. Rais katupa moyo na kutuhimiza tumalize kazi haraka na
tuifanye kwa weledi huku tukiweka maslahi ya Taifa mbele. Hata pale
alipotoa maoni na ushauri kuhusu baadhi ya vifungu bado Mh.Rais
alisisitiza kwamba uamuzi wa mwisho ni wetu sisi Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.
Tano, dhana ya kuichambua na
kuikosoa rasimu maana yake si
kumdhalilisha Mwenyekiti wa Tume na Wajumbe wake. Msingi mzima wa
kutolewa Rasimu hii ni kwamba
Wananchi tuichambue, tuikosoe,
tuirekebishe, tuiboreshe na hata ikibidi tuibadilishe na mwisho tutaipigia kura sote kwa pamoja. Rasimu haikuletwa kama Msahafu wala Biblia na ndiyo maana zimewekwa hatua mbili baada ya kazi ya tume kukamilika:
BUNGE MAALUM LA KATIBA na KURA YA MAONI YA WANANCHI.
Rais akiwa mkuu wa Nchi, naye ana nafasi yake katika mchakato wa Katiba. Sisi wana TANZANIA KWANZA, tunashukuru kwamba Mh. Rais alitutanabahisha kuhusu maeneo muhimu ya kuzingatia ambayo Tume haikuyaainisha kwa upana wake ikiwemo mipaka ya Nchi
yetu. Tunawapongeza Wajumbe wa tume kwa kazi waliyoifanya na kuikamilisha.
Kazi inayofuatia sasa ni uchambuzi wa Rasimu waliyoiwasilisha. Katika hatua hii ya sasa ya Bunge la Katiba, Rasimu hii inaweza ikakosolewa na hata inaweza kubadilishwa sana.
Tunawasihi Wajumbe wa Tume waondokane na dhana kwamba kazi yao inapojadiliwa tofauti na mapendekezo yao siyo udhalilishaji wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Sita, Sisi Wajumbe wa Bunge Maalum, wana TANZANIA KWANZA ambao idadi yetu ni zaidi ya Wajumbe 400 na ambao orodha yetu tutaitoa hivi karibuni kwa
wingi wetu na umoja wetu tunayo
dhamira ya kutimiza wajibu wetu kwa mujibu wa Sheria na kwa kuzingatia matarajio ya Watanzania.
Tunawasihi wale wenzetu ambao hawakuipenda hotuba ya Mheshimiwa Rais watulie, waondoe hamaki na sote tushirikiane kuifanya kazi hii, kama wapo ambao kitendo cha Rais kuja kuhutubia na kutoa uchambuzi wake kuhusu Rasimu, kinawafanya wasitake tena kushiriki
katika mchakato huu, basi uamuzi wao huo waufanye kwa namna ambayo haitatukwaza au kutuzuia sisi wengine tunaotaka kuendelea na shughuli hii ya mchakato wa Katiba.
Tunawasihi viongozi wa Bunge Maalum wasivumilie wala kuendekeza vitendo vya vurugu za
makusudi vitakavyozuia uendeshaji wa Bunge. Tunawasihi msiruhusu watu wachache wakaliweka rehani Bunge Maalum ili kutengeneza mtaji wa kisiasa.
Tunawasihi Watanzania wawaone na kuwahukumu wale watakaotaka kuvuruga au kukwamisha mchakato adhimu wa kupata Katiba mpya kisa tu Mh. Rais kaja kuhutubia Bungeni.
Mwisho, tunapenda kusisitiza kuhusu umuhimu mkubwa wa vyombo vya habari katika mchakato huu. Hiki ni kipindi muhimu sana katika uhai wa Taifa letu. Wananchi wengi wanafuatilia mchakato huu kupitia vyombo vya habari.
Tunawasihi wamiliki, wahariri na waandishi wa habari wazingatie
weledi wa hali ya juu sana katika
kuripoti mchakato huu. Wananchi
wanapenda kusikia, kuona na kusoma yanayojiri wala sio propaganda za wanasiasa au makundi mbalimbali.
Tunapenda kuvisihi vyombo vya habari viwaunganishe Watanzania wote katika kipindi hiki muhimu na cha kihistoria.
Hata hivyo tunatoa shukrani zetu za
dhati kwa vyombo vya habari na wanahabari wote kwa ushiriki wao
katika mchakato huu wa Katiba. Tunazidi kuwasihi waendelee kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa, kutokufanya kazi kwa kufuata propaganda za kisiasa au kufuata makundi, kutoa mizania sawa kwa maoni tofauti bila kuegemea maoni ya kundi moja au matakwa ya makundi fulani kwa kuwa mwisho wa siku sisi sote tuna jukumu kubwa la kuhakikisha tunakuwa na Tanzania moja.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Libariki Bunge Maalum la Katiba
“TANZANIA KWANZA”
Tunawashukuru kwa kutusikiliza.
Kwa niaba ya Wabunge wa Bunge la Katiba “WANATANZANIA
KWANZA”
The chairman of the Constituent Assembly, Mr Samuel Sitta, today embarks on what could be his baptism of fire since his election to the sensitive position over a week ago.Mr Sitta will attempt to solve one of the thorniest issues yet to bedevil the CA, with the 629 members so far failing to agree on what mode of voting should be adopted by the assembly.
The matter was so divisive that it was left pending when the committee that formulated the CA regulations under Prof Costa Ricky Mahalu presented its report.
Not even a reconciliatory team named by the then interim chairman, Mr Pandu Ameir Kificho, could break the deadlock on the method of voting.
Many CA members and independent commentators view how Members the Constituent Assembly (MCAs) should vote as an important weapon in winning in sticky points of the new constitution making process in the face of any stark political differences or vested interests.
Some MCAs have told The Citizen that the high stakes on whether an open or secret vote should prevail has been heightened by early signs that the ruling CCM was hell bent on pushing its own agenda.
“We know CCM has a direct interest with the open voting system with President Kikwete and Mr Sitta having already taken sides on this. Therefore the MCAs shouldn’t allow it to happen,” Mr John Mnyika told The Citizen yesterday.
Mr Mnyika, who is also the Ubungo MP from the opposition Chadema, cautioned that adopting an open voting system would mean CCM will bulldoze its way through. “It will kill democracy and public interest at the altar of political demigods,” he said.
While those who overwhelmingly voted for Mr Sitta say he should be given the benefit of doubt to remain neutral, others argue his CCM membership, and the President’s weekend address to the CA that left little doubt what he expects of the process – lives him with little room to manoeuvre.
“Sitta is now faced with making a tough decision to either side with CCM that has expressly told its MPs and other inclined members to settle for nothing other than open voting,” said a CCM member who asked not to be named due to the sensitivity that his party has attached to those it viewed as ‘rebels’ advocating the secret vote.
He said a secret vote will enable members make independent decisions. “Some of us from CCM have not been swayed by President Kikwete’s position and will not change the resolve to back secret vote,” said the MP from the Lake Zone.
He advised that Mr Sitta to look for a mutual consensus on the matter before proceeding. Mr Sitta was not immediately available yesterday for comment but soon after his election, he was quoted as pledging to steer the house fairly, and that he will be guided by the wider interest of the nation.
He pledged last Friday that stalemate on the voting method will be resolved this week ahead of naming of various committees to embark on the job proper.
Mr Mnyika pleaded with fellow MCAs to defeat any party propaganda and instead defend their right of a secret vote.
However, he added that the decision to go for open or secret vote will depend on who will become the steering committee chairperson. He added that the decision will also depend on who will be selected to join the chairman’s advisory committee.
Mr Ezekiah Oluoch said MCAs had already agreed to reach a consensus by sidelining selfish interests.
“I cannot speak for others but I believe in the secret vote…. this will ensure privacy and security to all MCAs,” the trade unionist said.
Yesterday, CCM’s publicity and ideology secretary, Mr Nape Nnauye, said the CA should be left alone to decide on the matter.
Sunday, March 23, 2014
BREAKING NEWS : MBUNGE WA NZEGA HAMISI KIGWANGALLA ANUSURIKA KUUAWA NA POLISI, HIKI NDO ALICHOKISEMA
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKOTOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Monday, March 17, 2014

Henry Kilewo Ameandika yafuatayo katika Ukurasa Wake wa Facebook kuhusu Uchaguzi wa Jana katika Jimbo la Kalenga Ambapo CCM waliibuka Washindi:
"Mapambano yanaendelea,hatujafa moyo, hatujahuzunika na wala hatutarudi nyuma, safari ndiyo inaanza kuwa na chachu ya mafanikio huku tukiendelea kuwa imara na kuimarika zaidi... wanakalenga tutaendelea kuongea na nyie na tunajua maamuzi yaliyofanyika yalikuwa siyo yenu bali Tume ya Taifa ya uchaguzi iliamua kuucheza mchezo mchafu pamoja na jeshi la polisi.
Hatujashindwa na kamwe hatutashindwa wala kukubali kushindwa pasipo na mazigira huru"
Mjumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, Tundu Lissu amesema ktendo cha Mwenyekiti wa Bunge la Katiba kubadilisha kanuni kwa kutoa muda zaidi wa kuwasilishwa kwa rasimu ya katiba, kinamkera.Lissu alisema kitendo kama hicho ndicho kilichomfanya yeye na mjumbe mwenzake, Ismail Jussa kutaka kujiuzulu mara mbili kutokana na kupingana na wajumbe wenzao.
Akizungumza na gazeti hili jana mjini hapa, Lissu alisema walitaka kujiuzulu kutokana na kuchoshwa na wajumbe kufikia makubaliano ndani ya vikao, lakini wakitoka nje wanarudi na mabadiliko.
“Tulikuwa hatusongi mbele tunafanya uamuzi na kufikia makubalino, lakini wenzetu baadaye wanaenda kujadiliana upya na kuja na mapendekezo tofauti na kuturudisha nyuma,” alisema Lissu.
“Baada ya majadiliano yao, mimi na Jussa tuliomba tujiondoe lakini walituomba tusijiuzulu kwa masharti kuwa tunachokubaliana hawataweza kubadilisha.”
Alisema kile ambacho kimeanza kutokea sasa ni kitendo cha Mwenyekiti Sitta kubadilisha kanuni ya 47 (a) ya Bunge hilo juu ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kupewa muda unaofaa kuwasilisha rasimu katika Bunge Maalumu la Katiba.
Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), alisema pia hata kubadilisha kanuni kwa kupokea kwanza taarifa ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na baadaye ndipo Rais Jakaya Kikwete azungumze ni jambo wanalolipinga.
Kushindwa kishindo kwa Chadema kunaelezwa kuwa kipigo kikubwa kwa chaguzi za hivi karibuni kwani wameshindwa kupata hata asilimia 20 .
See you Chalinze kuna kibano kinawasubiri.....
Dodoma. Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye amekata rufaa Kamati Kuu ya CCM kupinga adhabu ya onyo kali aliyopewa na chama kutokana na madai ya kuanza kampeni za urais mapema kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.
Akizungumza na gazeti hili mjini Dodoma jana, Sumaye alisema kwa ufupi hakuridhishwa na adhabu hiyo na kuthibitisha hilo, tayari amekata rufaa.
Hata hivyo, alisema hadi jana hakuwa amepata mrejesho wowote kwa sababu kanuni hazielezi ni muda gani anatakiwa kuwa amepewa taarifa kuhusu rufaa hiyo.
Sumaye na wanachama wenzake, Edward Lowassa, Bernard Membe, Stephen Wassira, William Ngeleja na January Makamba walitiwa hatiani kwa kuanza kampeni mapema, hivyo kupewa onyo linalokwenda sambamba na kutowania nafasi yoyote ndani ya chama kwa miezi 12.
“Siwezi kuwazungumzia wenzangu, nazungumza kwa upande wangu, sikuridhishwa na adhabu hii na nimeshakata rufaa ingawa sijapata majibu yoyote, naendelea kusubiri,” alieleza Sumaye.
Waziri Sumaye alikataa kuzungumzia hali ya utekelezaji wa adhabu hiyo, akisema anachosubiri ni mwitiko wa rufaa yake aliyoiwasilisha Kamati Kuu ya CCM, mwanzoni mwa mwezi huu. “Sina kumbukumbu nzuri ilikuwa tarehe ngapi, lakini ni mwezi huu wa tatu.”
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa juu ya rufaa hiyo alisema hana taarifa zaidi ya habari hizo kuzisikia kutoka kwa mwandishi.
Hata alipotakiwa kueleza nani anatakiwa kuwa na taarifa hizo, alisema: “Mimi ndiye msemaji wa chama, hakuna wa kuzungumzia suala hili zaidi yangu. Kwanza inatakiwa ijulikane, rufaa hiyo imepelekwa ngazi gani ya uongozi kwa sababu kila ngazi ina muda tofauti wa kufanya vikao vyake vya uamuzi.”
Nnauye baada ya kuelezwa kuwa rufaa ya Sumaye imewasilishwa Kamati Kuu ya CCM, alisisitiza kuwa hana taarifa nayo na kwamba haiwezekani rufaa ipelekwe kwenye kikao kilichotoa adhabu husika.
Hata hivyo, Sumaye alisisitiza kuwa rufaa yake ameiwasilisha Kamati Kuu kwa mujibu wa kanuni zinazohusika.
Friday, March 14, 2014
Jengo la makao makuu ya CHADEMA yaliyopo mtaa wa ufipa Kinondoni yameviwa ma vijana waendesha boda boda wa jijini Dar muda huu wakitaka waonane na viongozi wa chama hicho kuwaeleza kero na manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa maofisa wa jiji pamoja na askari polisi katika utekelezaji wa mujukumu yao ya kujipatia riziki.
Kutokana na hali hiyo tayari polisi wameshazingira eneo zima la makao makuu ya CHADEMA kwa ajili ya tahadhari ya jambo lolote
Wednesday, March 12, 2014
Tuesday, March 11, 2014

Mara baada ya mbunge mmoja kusimama na kumuomba Mwenyekiti wa Bunge Pandu Ameir Kificho awatake watendaji wake wagawe vikaratasi vya kura ili ipigwe kura ya siri wachaguwe aidha siri au wazi na kuondokana na kanuni hizo zilizodumumu takriban siku kadhaa bila ya kupatiwa ufumbuzi na wajumbe wengi kuunga mkono.
Mh Ole Sendeka ameonyeshwa na kamera za bungeni akiwa amebeba mafail yake na kutoka nje ya ukumbi wa bunge huku akifuta futa machoz.
Dodoma, Tanzania. Mchungaji Christopher Mtikila amechafua hali ya hewa bungeni, hivi punde kwa kumtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Pandu Kificho amueleze ni kwanini tangu jana amekuw akimnyima nafasi ya kuzungumza bungeni.
Mchungaji Mtikila alisimama ghafla na kusema: Mwenyekiti kwanini unaninyima haki yangu ya kuzungumza, nataka kujua kwanini unaninyima haki ya kuzungumza. Kuzungumza ni haki yangu."
Mchungaji Mtikila amezungumza kwa jazba huku wajumbe wengine wakimzomea, lakini bila uwoga aliendelea kuzungumza na kusema yanayofanyika Mungu anapenda na yeye ana amini katika Mungu, lakini "Wewe Mwenyekiti inaonekana kuwa hupendi Mungu."
Wakati Mchungaji Mtikila akimwakia Kificho, Felix Mkosamali alilipuka na kumwambia mwenyekiti kuwa tangu jana pia anamnyima nafasi.
"Ninyi mmejipanga, kupitisha kanuni mbovu, alafu sisi wengine hamtupi nafasi," amesema Mkosamali.
Mwenyekiti Kificho aliwajibu kuwa kwa bahati mbaya wamekosa nafasi na hivyo wawe wavumilivu.
Kificho anatangaza utaratibu wa kumchagua Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge na wajumbe wanaotaka kugombea nafasi hiyo wametakiwa kuchukua fomu ya kugombea.
Bunge hilo limeahirishwa mpaka kesho na kanuni zitaanza kufanya kazi rasmi.












