Tuesday, March 11, 2014
LOWASSA AIKANA NOTI YA SH 500 YENYE PICHA YAKE BADALA YA RAIS
Tuesday, March 11, 2014 by Unknown
Kumekuwa na muendelezo wa matukio kadhaa kutoka kwa kikundi cha watu kumuhusisha Mhe. Edward Lowassa na matukio ya uongo na kumzushia vitu vya ajabu kabisa, hususani katika mitandao ya kijamii.
Kumesambazwa picha ya noti ya shilingi mia tano yenye picha ya Mhe. Lowassa. Kitendo hicho siyo utani, bali ni dhihaka na dharau kwa alama za Utaifa na Mamlaka ya nchi. Lowassa Amesema hajui na wala ahusiki na usambazaji wa Noti hiyo Mitandaoni
Mhe. Lowassa anaheshimu maoni ya watu na nguvu ya mitandao ya kijamii, lakini anasisitiza umuhimu kwa wananchi kutumia nguvu hiyo ya mitandao kwa kujadili maendeleo ya nchi yetu badala ya kuwa watu wa kuzusha mambo yasiyo na tija kwa nchi yetu.
Imetolewa na:
Ofisi ya Mhe. Lowassa (MB)

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 Responses to “LOWASSA AIKANA NOTI YA SH 500 YENYE PICHA YAKE BADALA YA RAIS”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.