Monday, March 17, 2014
JERRY TEGETE"YANGA HAUNA CHAKO RUDI SHULE AMA UHAME TEAM"
Monday, March 17, 2014 by Unknown
BABA mzazi wa straika wa Yanga Jerry Tegete, John Tegete amemtaka mwanae achague mawili ifikapo mwisho wa msimu huu iwapo ataendelea kusugua benchi kwenye kikosi hicho.
Kocha huyo wa zamani wa Toto African ya Mwanza alisema kuwa mbali na ukocha yeye pia ni mzazi hivyo lazima afuatilie maendeleo ya mwanae.; “Naona mwanangu hana bahati na Yanga, licha ya kucheza michezo minne na kufunga mabao matano. Naamini bado anaweza kucheza na kupachika mabao, lakini kama hana nafasi basi nampa hadi mwisho wa msimu aweze kuamua kati ya kusoma au kucheza soka nje ya Yanga,” alisema.
Kama ni kurudi shule basi Jerry ni kati ya wachezaji watakaokuwa na elimu zaidi kwenye soka la Tanzania kwani tayari ni mhitimu wa kidato cha nne. Lakini amefunikwa kielimu na Reliants Lusajo mwenye Digrii ya ugavi, Salum Telela anayesoma Digrii ya Biashara na Issa Ngao naye anayesomea biashara.
SOURCE: MWANASPOTI Tags: michezo

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 Responses to “JERRY TEGETE"YANGA HAUNA CHAKO RUDI SHULE AMA UHAME TEAM"”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.