Monday, March 17, 2014

"SIWEZI KUINGIA MAPENZINI NA MSANII WA BONGO MOVIES..WENGI WAPO KIMASLAHI"MBOTO




Muigizaji wa filamu za Kiswahili, Haji Salum aka Mboto amesema kuwa hawezi kuanzisha uhusiano wa mapenzi na wasanii wa Bongo Movie kwa kuwa anaogopa kuchafuliwa jina na kuumizwa kimapenzi.

Mboto alifunguka kupitia mahojiano maalum na Zourha Malisa, ambapo amedai kuwa wasanii wengi wa kike wa filamu za kitanzania (Bongo Movies) hawana mapenzi ya kweli na kwamba wengi wanaangalia maslahi zaidi.

Hata hivyo, alieleza kuwa hatamani kuwa na uhusiano na baadhi ya wasanii hao, bali inamlazimu kuzuia hisia zake ili kuepuka mambo mbalimbali yatakayoyumbisha maisha yake.

"Unajua mimi pia nina tamani na pengine wao wananitamani ila najizuia na wala sitaki kuruhusu majaribu kwani najua ninachokifanya huku kwenye tasnia yetu tunakijua hivyo ni lazima ujiepushe na mambo mengine." Alisema Mboto.

Ameeleza kuwa kuna waigizaji wengi wa kike ambao ni rafiki zake wa karibu na wanashirikiana vizuri kwenye kazi.

Tags:

0 Responses to “"SIWEZI KUINGIA MAPENZINI NA MSANII WA BONGO MOVIES..WENGI WAPO KIMASLAHI"MBOTO”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI