Thursday, November 21, 2013
IVO MAPUNDA : JUMA KASEJA BADO NI KIPA BORA TANZANIA
Kipa wa Taifa Stars na Gor Mahia, Ivo Mapunda amemtoa wasiwasi mwenzake Juma Kaseja kwa kumwambia ‘wewe bado ni Tanzania one’.
Mapunda alisema uamuzi wa Kaseja kwenda Yanga ni sahihi na kumtaka atulize akili ikiwezekana atafute watu wa saikolojia kwa ajili ya kumpa ushauri.
“Kaseja ni kipa bora, wanaosema ameshuka kiwango nawashangaa watakuwa hawajui vizuri soka,”alisema Mapunda.
Alisema,”Yanga wamelamba dume, atawasaidia, mimi binafsi namkubali, yupo kwenye kiwango kizuri, ana uzoefu wa muda mrefu Simba watajutia kumuacha.”
“Mimi namuomba Kaseja atulize akili, mimi mbona walisema nimekwisha sina jipya, lakini mbona nipo kwenye fomu nina uwezo wa kucheza hata miaka 10 mbele, kikubwa ni nidhamu ya mazoezi na kujitunza,”alisema Mapunda.
Kauli ya Ivo imekuja baada ya Kaseja kumwaga wino wa kuichezea Yanga kwa kitita cha sh 40 milioni baada ya kukaa nje kwa muda. Kaseja alisajiliwa Simba mwaka 2003 akitoka Moro United na tangu wakati huo alikuwa kipa tegemeo wa Simba kwa misimu tisa ingawa kwa msimu mmoja wa 2008/2009 aliichezea Yanga kabla ya kurudi tena Simba.

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.

0 Responses to “IVO MAPUNDA : JUMA KASEJA BADO NI KIPA BORA TANZANIA”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.