Wednesday, March 26, 2014

YANGA NA AZAM WAZIDI KUKABANA KOO..WOTE WASHINDA LEO



 
Vilabu vya Azam FC na Yanga SC leo vimeendelea kukabana koo katika mbio za ubingwa wa ligi kuu Vodacom baada ya vyote viwili kupata ushindi kwenye michezo yao waliyokuwa wakicheza leo hii.
Azam FC ikiwa katika dimba la Mkwakwani ilikuwa ikicheza na Mgambo JKT na matokeo ni kwamba wamefanikiwa kushinda kwa magoli 2-0.
Magoli ya Azam yalifungwa na Brian Omony na John Bocco Adebayor.
Kwa upande wa Yanga ambao leo walikuwa wakicheza na Tanzania Prisons kutoka Mbeya katika uwanja wa taifa – matokeo ni Yanga wameshinda 5-0.
Magoli ya Yanga yalifungwa na Emmanuel Okwi, Mrisho Ngassa, Hamis Kiiza alifunga mawili na nahodha Nadir Haroub Cannavaro aliyefunga kwa penati.

Tags:

0 Responses to “YANGA NA AZAM WAZIDI KUKABANA KOO..WOTE WASHINDA LEO”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI