Wednesday, March 27, 2013

BARRICK YATOA TUZO KWA WAFANYAKAZI BORA




Simon Shayo, mfanyanyazi wa Mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold (ABG) akiwa na tuzo ya ufanyakazi bora kwenye idara ya mahusiano ya jamii kwenye sherehe zilizofanyika mgodini hapo Machi 21, 2013. Shayo na timu nzima ya mgodi huo wamepewa tuzo hiyo kutokana na mradi wa kusaidia kikundi cha wanawake cha Nyabichune kijikwamue kiuchumi.Igor Gonzales, makamu wa rais mtendaji na afisa mwandamizi (Executive Vice President & Chief Operating Officer) wa kampuni ya Barrick Gold Corp. (kushoto), akitoa zawadi ya tuzo ya mfanyakazi bora kwa Godfrey Nyabuzoki, mfanyakazi wa kitengo cha ulinzi cha mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold kwenye sherehe iliyofanyika Machi 21,2013. Godfrey na wafanyakazi wengine watano wa kitengo cha ulinzi cha mgodi huo walionesha ujasiri mkubwa kukabiliana na kundi kubwa la wananchi waliovamia mgodi huo mwezi Machi mwaka huu na wafanyakazi hao wakaweza kumuokoa mwenzao aliyeumia. Kulia ni makamu wa rais wa kampuni ya Barrick Gold Corp. anayeshughulikia masuala ya ulinzi, Mark Wall.

Marco Zolezzi, afisa mwandamizi (Chief Operating Officer) wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold, akitoa zawadi ya tuzo ya mfanyakazi bora kwa mfanyakazi wa kitengo cha uchunguzi cha mgodi wa Bulyanhulu, Gilbert Kalisa, kwenye sherehe zilizofanyika Machi 21, 2013, kwenye mgodi huo.

Tags:

0 Responses to “BARRICK YATOA TUZO KWA WAFANYAKAZI BORA ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI