Sunday, March 24, 2013
Rose Muhando kutambulisha mambo mapya Pasaka
Sunday, March 24, 2013 by Unknown
Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI nguli wa muziki wa kiroho, Rose Muhando amejipanga kisawaswa katika Tamasha la Pasaka mwaka huu na anatarajia kutambulisha albamu yake mpya iitwayo Tazama Mungu Anacheka.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema Dar es Salaam jana kuwa mwimbaji huyo amemuhakikishia kuwa amewaandalia mashabiki wake vitu vikubwa kwenye tamasha hilo litakalofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Jumapili wiki hii na siku inayofuata Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Msama alizitaja nyimbo zilizopo katika albamu hiyo kuwa ni Mungu Anacheka, Tenda Wema, Mungu Unshangaza, Mwanamke Mbaya, Sema Nami, Penye Raha,Heri Wenye Moyo, Shujaa wa Msalaba na Tembea Baba.
Akizungumzia maandalizi ya onesho hilo, Msama alisema yanaenda vizuri na kwamba wasanii wan je ya nchi wanatarajiwa kuanza kuwasili Alhamisi wiki hii na kuwaomba mashabiki wakae mkao wa kula kupata mambo mazuri.
Wasanii wan je ya Tanzania watakaotumbuiza ni kundi la Ambassadors of Christ ‘Kwetu Pazuri’ la Kigali, Rwanda ambalo pia linatarajia kuzindua albamu yao mpya iitwayo Kaeni Macho. Wasanii wengine wa nje ya Tanzania watakaotumbuiza tamasha hilo ni Sipho Makhabane wa Afrika Kusini, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya.
Wasanii wa Tanzania waliothibitisha licha ya Rose Muhando ni Upendo Nkone, John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival, Bonny Mwaitege, Upendo Kilahiro na kundi la Glorious Celebration
Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31 na litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Rose Muhando kutambulisha mambo mapya Pasaka”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.