Monday, March 18, 2013

TUPO PAMOJA KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO ILIVYO RINDIMA MITAA YA JIJI LA DAR ES SALAAM


Kampeni Kabambe ya kuitangaza Bia ya SerengetiLager inayozalishwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ijulikanayo kama TUPOPAMOJA KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO imelitikisa mitaa na vitongoji vya jiji la Dar es Salaam jana.


Huku pakiwa na burudani ya muziki ambayo
iliashiria Shangwe za mafanikio, Msafara wa magari kadhaa ya Kampuni ya Bia ya
SBL pamoja na Lori kubwa aina ya Scania Semitrailer likiwa limepambwa vilivyo
na kuleta mvuto wa ajabu kwa Watanzania lilikatika mitaa mbalimbali ya jiji.

Msafara huo wa kutoa Shukrani kwa Watanzania
ndani ya jiji la Dar es Salaam ulianzia katika Kiwanda cha SBL Temeke kisha kwenda
hadi Mwembeyanga hadi Saba saba.

Shangwe hizo ziliendelea hadi Taifa, Chang’ombe,
Kamata, Msimbazi, kisha msafara huo ukaingia baranbara ya uhuru, ukapita Ilala
ukaja tokea Buguruni, ukaingia Barabara ya Mandela hadi Ubongo kisha ukapita Kituo
Kikuu cha Mabasi Ubungo, ukaelekea Sinza ukatokea Bamaga ukafuata barabara ya
Bagamoyo hadi Victoria ukaingia Mwananyamala na kumalizia viwanja vya Biafra
Kinondoni.
Aidha shsngwe hizo zilikuwa zikiendelea katika
maeneo kadhaa ya sehemu za starehe za Miti Mirefu, Kimara, Jambo park jet Lumo,
Huduma Mbagala na Airtel Pub Banana.
Magari kadhaa ya Kampuni ya Bia ya Serengeti yaliongoza msafara huo.


Ni mwendo wa Shangwe tu ulikuwa ukiemdxelea kila kona Gari hilo lilipopita. Mbali na kampeni hii katika Mitaa ambayo imeanzia
jijini Dar es Salaam na pia itasambaa mikoani pia Matangazo katikia vituo vya
televisheni, Redio, Magazeti na Blogs yatakuwa yanatoka pamoja na mitaani.




Magari mengine yalikuwa Nyuma na kupambwa na chapa mbalimbali za Bidhaa za kampuni ya SBL.
Tupo Pamoja katika Shangwe za Mafanikio…

Tags:

0 Responses to “TUPO PAMOJA KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO ILIVYO RINDIMA MITAA YA JIJI LA DAR ES SALAAM ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI