Monday, April 8, 2013

Tangazo Maalum Kutoka Bohadi ya Madawa:Watumishi wa vituo vya afya na zahanati nchini, wametakiwa kuwasilisha mapema oda zao za dawa kwa waganga wakuu wa wilaya mwishoni mwa juma la kwanza la mzunguko wa ugavi shirikishi




Watumishi wa vituo vya afya na zahanati nchini, wametakiwa kuwasilisha mapema oda zao za dawa kwa waganga wakuu wa wilaya mwishoni mwa juma la kwanza la mzunguko wa ugavi shirikishi.

Hayo yamesemwa leo na KAIMU Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani alipokuwa akizungumza na wakurugenzi wa halmashauri, waganga wakuu, wafamasia pamoja na wawakilishi kutoka taasisi za Mashirika ya Dini.

Mwaifwani alisema utaratibu huo utawawezesha MSD kutumia majuma nane kuchambua oda, kutengeneza Ankara za mauzo na kuzifungusha na kuzifikisha dawa moja kwa moja kituo cha afya na zahanati ifikapo juma la kumi na mbili.

“ili tuweze kuwahudumia kwa kiwango kizuri tunahitaji hospitali ziwasilishe mahitaji yake siku kumi na nne kabla ili sisi tuweze kujiandaa vya kutosha na kukamilisha oda kwa wakati”.

Aidha,alisema kuwa, malalamiko mengi ya kutokuwa na dawa katika vituo vya afya nchini, yanasababishwa na watendaji wasio waaminifu ambao hawazifikishi vituoni.
Mwaifwani alisema hayo Pia alisema wengine huziuza kwenye maduka ya dawa ya watu binafsi ili kujipatia utajiri wa haraka haraka.

“Ili kuzuia mwanya huu, MSD itakuwa inafikisha dawa hadi ngazi ya zahanati na vituo vya afya nchini nzima kuanzia Julai mwaka huu,” alisema.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, kunapokuwepo na shida ya utendaji au ushauri wowote kuhusu MSD inapaswa kuzitumia ofisi zao za kanda zilizopo nchini nzima, mteja asiporidhika malalamiko hayo yapelekwe katika ofisi yake.

Awali Meneja wa MSD kanda ya Kaskazini, Celestine Haule alisema kuwa, bohari kuu ya dawa nchini ilipewa agizo na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii la kufikisha dawa, vifaa tiba na vitendanishi hadi ngazi ya zahanati.

Alisema lengo lilikuwa ni kupunguza mlolongo mrefu uliopo kwa sasa katika ufikishaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya kutolea huduma ya afya.

Mwisho

Na. 
Catherine Sungura, 
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Morogoro 8/4/2013

Tags:

0 Responses to “Tangazo Maalum Kutoka Bohadi ya Madawa:Watumishi wa vituo vya afya na zahanati nchini, wametakiwa kuwasilisha mapema oda zao za dawa kwa waganga wakuu wa wilaya mwishoni mwa juma la kwanza la mzunguko wa ugavi shirikishi ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI