Thursday, April 11, 2013
Waziri Mulugo Kuwafkisha Mahakamani wanaodai kuwa Ameghushi vyeti
Thursday, April 11, 2013 by Unknown
Mulugo alitoa kauli hiyo alipofungua mkutano wa mwaka wa Umoja wa Wamiliki wa Shule za Sekondari na Vyuo Binafsi Tanzania (TAMONGSCO0) jijini Mbeya.
“Wanasema eti nimeghushi vyeti, mara ooh sijui natumia jina la mtu. Nimechoshwa na maneno haya… ni kweli nimerudia darasa kama walivyorudia watu wengine, kwa nini iwe tatizo kwangu. Hata hapa tulipo wapo wengi tu waliorudia darasa.
“Kama kweli ningekuwa nimeghushi vyeti hivi leo ningekuwa naibu waziri wa elimu? Sasa nimechoshwa, nitawachukulia hatua watu hawa, siwezi kusema ni lini nitafanya hivyo ila nitakapoamua nitaanza,”alisema.
Kwa miezi kadhaa sasa Mulugo amekuwa akidaiwa kughushi vyeti na kutumia jina la mtu ili kufikia kiwango cha elimu alichonacho madai ambayo alisema yanamchafulia jina katika jamii.
Kuhusu suala la matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana, Mulugo alisema matokeo hayo mabaya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na mmomonyoko wa maadili miongoni mwa wanafunzi.
Naye Ruth Mnkeni kutoka Dar es Salaam anaripoti kuwa Mlugo amezindua tovuti ya elimu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ijulikanayo kama Shule Direct.
Muluigo alisema kuzinduliwa kwa tovuti hiyo kutawafanya wanafunzi kupata maarifa mengi ya vitabu mbalimbali na kuinua kiwango cha elimu nchini.
This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Waziri Mulugo Kuwafkisha Mahakamani wanaodai kuwa Ameghushi vyeti”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.