Sunday, April 7, 2013
Wote Wanaoipinga Redio ya watu Clouds Fm wana Chuki Binafsi
Kwa mda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia mijadala mbalimbali zinazohusu radio ya watu claus.watu weng mmekuwa vinara wa kuiponda pamoja na watangazaji wake.nilichogundua hakuna hoja ya maana mnayotoa juu ya redio hii pendwa. Mimi nashauri tuache unafiki na kuwa watu wanaokubali mafanikio ya wengne. Ktk kipindi cha miaka kumi mfululizo redio hii pendwa imejizolea mashabiki ndani na nje ya nchi. Mafanikio yao yametokana na kujua mahitaji ya wasikilizaji. Kwa kifupi ni wabunifu sana katika vipindi vyao. Haishangazi hadi kupata hadh ya super brand radio station. Na hii ndiyo sababu inayofanya iwe na mapato makubwa kupitia mikataba ya matangazo kuliko hata east africa radio. Vipindi vya kijanja kama xxl,leo tena,jahazi,bongo fleva vina mashabiki wengi kuliko vya redio pinzani(ea radio) kama power jam,ea breakfast,planet bongo.ina watangazaji wabunifu kama b12,adam mchomvu,fetty ambao wamekuwa kipenzi cha vijana wengi ambao ndio wasikilizaji wakubwa. Pia ni waandaaji wa tamasha kubwa la fiesta ambalo linahesabiwa kuwa tamasha kubwa zaidi east africa.
MAONI YANGU.
Tumsifie anayefanya Vema na Si kumponda..Wengi wetu tunaoikosoa ndo wasikilizaj wazuri wa radio hii pendwa.sijatumwa na kibaraka yoyote haya ni mawazo yangu chanya najua mtaniponda kwa mawazo yenu mgando
VIVA CLOUDS FM...the pipoz station.
This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
0 Responses to “Wote Wanaoipinga Redio ya watu Clouds Fm wana Chuki Binafsi”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.