Thursday, April 11, 2013

XAVI HERNANDEZ APIGA PASI 96 KWENYE MECHI DHIDI YA PSG - AWEKA REKODI YA KUTOPOTEZA PASI HATA MOJA KWENYE CHAMPIONS LEAGUE


Haukuwa mchezo mchezo ambao Barcelona walionyesha kiwango kikubwa, lakini Xavi alikuwa na usiku mzuri kuliko: akipiga pasi 96 na zote zikiwa zimewafikia walengwa - kwa maana hakupoteza pasi katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Paris St Germain.  
Wakatalunya walikuwa kwenye hatari ya kukosa kucheza nusu fainali ya Champions League kwa mara ya 6 mfululizo baada ya kuwa nyuma baada ya dakika 50 ya mchezo huo, lakini wakaweza kurudisha goli dakika ya 71 likifungwa na Pedro.

Wengi watazungumzia kuhusu mabadiliko ya timu baada ya Messi kuingia, lakini ilikuwa ni Xavi aliyekuwa kwenye kiwango akikiongoza kiungo cha Barca kupeleka mashambulizi mbele aliyeleta utofauti mkubwa.

Mhispania huyo mwenye miaka 33, alicheza dakika 90 na kufanikiwa kutopoteza pasi hate moja - na kuweka rekodi mpya ambayo haijawahi kufikiwa na mchezaji yoyote.

Xavi aliweza kuipita rekodi ya Javier Zanetti dhidi ya Tottenham aliyoiweka miaka mitatu iliyopita, Emmanuel Eboue anashika nafasi ya taut kwenye list ya wachezaji waliopiga pasi nyingi kwenye mchezo mmoja.

Wakati mhispania akikaribia kutimiza pasi 100, Zanetti na Eboue walipiga pasi 72 na 54 katika me chi zao walizocheza. 


Wachezaji waliopiga pasi nyingi bila kupoteza katika Champions League tangu wa 2003/04 

MatchYearPlayerPasses
Barcelona v PSG2013Xavi96
Inter vs Tottenham2010Javier Zanetti72
FC Porto vs Arsenal2006Emmanuel Eboue54
Barcelona vs Stuttgart2007Lilian Thuram50
Real Madrid vs Man City2012Cristiano Ronaldo50
Braga vs Galatasaray2012Paulo Vinicius 48
Basel vs Barcelona2006Martin Caceres48
Chelsea vs Werder Bremen2008John Terry47
FC Porto vs Dynamo Kiev2006Rolando45
Roma vs Real Madrid2004Ivan Helguera43
Real Madrid vs Dinamo Zagreb2011Sergio Ramos43

Tags: ,

0 Responses to “XAVI HERNANDEZ APIGA PASI 96 KWENYE MECHI DHIDI YA PSG - AWEKA REKODI YA KUTOPOTEZA PASI HATA MOJA KWENYE CHAMPIONS LEAGUE”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI