Home
» michezo
» BAADA YA MTANDAO HUU KUTOA BARUA HALISI YA FIFA - TFF WATOA SIKU SABA SHAFFIH DAUDA KUTOA MAELEZO ALIPOITOA BARUA HIYO
Friday, May 10, 2013
BAADA YA MTANDAO HUU KUTOA BARUA HALISI YA FIFA - TFF WATOA SIKU SABA SHAFFIH DAUDA KUTOA MAELEZO ALIPOITOA BARUA HIYO
Friday, May 10, 2013 by Unknown
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtaka Shaffih Dauda ambaye ni mmiliki wa tovuti ya www.shaffihdauda.com kutoa maelezo kuhusiana na barua ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) aliyoiweka kwenye mtandao wake huo.
FIFA ambayo ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa TFF baada ya baadhi ya wagombea kuulalamikia, baadaye ilitoa maelekezo kuhusu mchakato huo kwa barua ambayo iliituma kwa Rais wa TFF, Leodegar Lenga.
Rais wa TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao Dauda alihudhuria alibainisha kuwa barua hiyo ya FIFA hawezi kupewa kila mtu, na kuruhusu waandishi kuisoma kwa Ofisa Habari wa TFF bila kuondoka nayo.
Wakati Rais Tenga anazungumza na waandishi wa habari (Mei 2 mwaka huu), nakala ya barua hiyo ya FIFA ilikuwa kwa viongozi wakuu wa TFF pekee, na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Hivyo TFF imemtaka Dauda kutoa maelezo ya mahali alipoipata barua hiyo ndani ya siku saba.
CREDIT www.shaffihdauda.com
Tags:
michezo
This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BAADA YA MTANDAO HUU KUTOA BARUA HALISI YA FIFA - TFF WATOA SIKU SABA SHAFFIH DAUDA KUTOA MAELEZO ALIPOITOA BARUA HIYO ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.