Monday, May 6, 2013
Babu wa Loliondo anaswa Benki.
Monday, May 6, 2013 by Unknown
Katika kuonesha kuwa Mchungaji Mstaafu, Ambilikile Mwasapile ‘Babu wa Loliondo’ bado ana fedha baada ya kuzikusanya kutoka kwa wateja wake wa huduma ya kikombe, hivi karibuni alinaswa ndani ya Benki ya NMB akipata huduma.
Babu alibambwa ndani ya benki hiyo Tawi la Loliondo mkoani Manyara akihudumiwa na mmoja wa wafanyakazi aliyefahamika kwa jina la Lembris Lesion ambapo inaelezwa alikuwa akielekezwa jinsi ya kujiunga na huduma mpya ya Jisevie.
Akiwa benki hapo, Babu alionekana akijaza fomu huku akiwa na begi ambalo linashukiwa kuwa na fedha ndani yake ambapo baadhi ya watu waliokuwa wakimpiga chabo hawakuonesha kumshangaa wakiamini bado ana mkwanja wa kutosha kutokana na ile tiba ailiyokuwa akiitoa kwa watu wengi hivi karibuni.
“Unajua Babu alipata pesa nyingi sana na bado anaendelea kuzikusanya, kimsingi ana pesa ndefu benki,” alisema mmoja wa wateja aliyekuwa eneo hilo. GPL
Tags:
udaku

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 Responses to “Babu wa Loliondo anaswa Benki. ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.