Tuesday, May 7, 2013
FBI WATUA RASMI ARUSHA KUCHUNGUZA MLIPUKO KANISA LA OLASITE
Tuesday, May 7, 2013 by Unknown
ASKARI wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), wamewasili mjini Arusha jana asubuhi kwa ajili ya kuongeza nguvu za kuwasaka watu waliohusika na mlipuko wa bomu katika Kanisa la Parokia ya Joseph Mfanyakazi Olasite.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo waliwaambia hayo wananchi eneo hilo jana jioni, wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliwatembelea kwa ajili ya kuwapa pole waumini wa kanisa hilo.
“Ndugu zangu, nawapa pole sana, Serikali yenu inakesha usiku na mchana, napenda kuwaambia leo (jana) tumepokea askari wa FBI hapa kwetu wamekuja kuongeza nguvu ya kuwasaka wahalifu hawa.
“Tunawaomba mwendelee kutusaidia kwa kila aina na taarifa zenu tutazifanyia kazi muda wote, tutahakikisha wote waliohusika wanatiwa mbaroni,” alisema Mulongo.
Kwa upande wake, Pinda alisema amesikitishwa na tukio hilo ambalo mpaka jana jioni limesababisha vifo vya watu watatu.
Alisema kwa wale wote ambao wamefariki, Serikali itagharamia mazishi yao kwa gharama na watazikwa kwa heshima zote zinazotakiwa.
“Nimemwagiza RC Mulongo, kuhakikisha wanafuatilia wale wote ambao wamefariki wanazikwa kwa gharam

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “FBI WATUA RASMI ARUSHA KUCHUNGUZA MLIPUKO KANISA LA OLASITE ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.