Home
» celebrities
» HAMMER Q AWAOMBA MSAMAHAMASHABIKI WAKE KWA ITENDO ALICHOKIFANYA CHA KUMPIGA MKE WAKE, ASEMA HATORUDIA
Saturday, May 11, 2013
HAMMER Q AWAOMBA MSAMAHAMASHABIKI WAKE KWA ITENDO ALICHOKIFANYA CHA KUMPIGA MKE WAKE, ASEMA HATORUDIA
Saturday, May 11, 2013 by Unknown
Ningependa kutumia muda huu kuandika kilichopo kataka moyo wangu na kifike kwa jamii yote iliyonizunguka ,
kikubwa zaidi nikuomba msamaha kwenu juu ya tukio nililolifanya wiki iliyopita, napiga magoti mbele yenu na kukiri kuwa nimewakosea nawaomba mnisamehe,
hata km ndani nimeshasamehewa lakini itakuwa siuungwana km sitawaomba msamaha wakubwa zangu pamoja na wadogo zangu sababu najua nilichokifanya kiliwauma na kuwakera sana sana mpaka nashindwa sema ni sana kiasi gani, lakini sitochoka kuomba msamaha kwenu na sitarudia tena, ,, kila mtu alisema lake hata kama alikuwa hajui wengine walipata kupendezesha vipindi vyao kwenye maradio na mablog pamoja na magazeti, mtihani wangu ulikuwa biashara kwao lakini simlaumu yeyote kwani nilifanya kitu cha kijinga na kisichokuwa na ubinadam,,
Si vibaya pia nikijiita mjinga, kwa sababu naweza nukuu maandiko yanayosema( HASIRA HUBEBWA NDANI YA KIFUA CHA MJINGA) siku zote maandiko hayakosei sababu Ndio tunayoyafuata, lkn pia.
Ninavojua muungwana ni kujitambua ulipokosea na kuomba msamaha kwani ukiomba msamaha hata mungu hukupa radhi zake nami niko mbele yenu naomba msamaha tena ,kwa kweli ni kipindi cha wiki moja iliyosheheni majuto na maumivu ya moyo na kuikosa amani , nilikuwa nahisi dunia yote imenielemea niliwaza vingi sn tena ni vibaya sana ila wife wangu alikuwa mstari wa mbele kunipa moyo hata km nilimkosea , roho ilikuwa inaniuma sana kuona niliemkosea anakuwa msaada kwangu kwa kila kitu na ninamshkuru kwa yeye kunisamehe naamini wapo wachache sn wenye moyo km wake , ama kweli hasira hasara na majuto ni mjukuu sababu yanakuja mwishoni kabisa Sikufanya kitendo kizuri mbele ya walimwengu mpaka mbele ya mungu lkn ss nataka niwe mpya kabisaaa. Mwisho kabisa shukran kwa kila alienisamehe na atakae nisamehe
nataka ktk kichwa chako ww unaesoma ujumbe huu kubaki kauli ya kuwa SITARUDIA TENA
This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HAMMER Q AWAOMBA MSAMAHAMASHABIKI WAKE KWA ITENDO ALICHOKIFANYA CHA KUMPIGA MKE WAKE, ASEMA HATORUDIA ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.