Wednesday, May 8, 2013

Hukumu ya Ponda kesho,kusuka ama kunyoa





Katibu wa Jumuia ya Kislamu Sheikh Ponda akiwa chini ya ulinzi mkaliDar es Salaam,Tanzania



HUKUMU ya kesi Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49 inatarajiwa kutolewa keshho. Sheikh Ponda na wenzake wanakabiliwa na kesi ya jinai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakidaiwa kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Chang’ombe Markazi, wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam.

Hukumu yao ilitarajiwa kusomwa Apri 18, mwaka huu na Hakimu Mkazi Viktori Nongwa, aliyekuwa akiisikiliza tangu mwanzao, lakini ilishindikana kutokana na hakimu huyo kutokuwepo.Badala yake iliahirishwa hadi kesho.

Akiahirisha kesi hiyo,Hakimu Mkazi Aloyce Katema alisema kuwa Hakimu Nongwa hayupo na kwamba hadi jana alikuwa hajaituma kwa ajili ya kusomwa (hakimu huyo alishahamishiwa mkoa mwingine wakati akiendelea kusikiliza kesi hiyo) hakuwa ameileta hukumu hiyo kwa ajili ya kusomwa.

Ponda na mwenzake, kiongozi wa taasisi ya jumuiya hiyo ya Waislam, Mukadamu Swalehe ambao ndio pekee waliobaki mahabusu baada ya dhamana yao kufungwa na Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP),walirudishwa mahakabusu hadi leo.

Ponda na wenzake wanakabiliwa na jumla ya mashataka manne kwa pamoja, huku Ponda na Swalehe wakikabiliwa na shtaka lingine moja peke yao. Mashtaka hayo yanayowakabili washtakiwa wote ni pamoja na kula njama za kutenda kosa, kuingia kwa nguvu katika eneo la ardhi la Chang’ombe Markaz, linalomilikiw ana kampuni ya Agritanza Limited.

Mashtaka mengine yanayowakabili washtakiwa wote ni, kujimilikisha na kukalia kwa nguvu eneo hilo la ardhi, na wizi wa vifaa vya ujenzi vyeny thamani ya Sh59.6 milioni, mali ya Agritanza Limited. Shtaka la ziada kwa Ponda na Swalehe ni la uchochezi, wakidaiwa kuwachochoea wafuasi wao kutenda Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati kati ya Oktoba 12 na 16, 2012, katika eneo la Chang’ombe Markaz, wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam.

Tags:

0 Responses to “Hukumu ya Ponda kesho,kusuka ama kunyoa”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI