Tuesday, May 7, 2013

Julio wa BBA Stargame aachia ngoma mpya ‘Mr Big Brother’


Pamoja na kwamba alidumu wiki moja tu kwenye shindano la mwaka jana la Big Brother Africa Stargame, aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania mwaka jana, Julio Batalia bado ana mapenzi mazito na shindano hilo kiasi cha kuachia wimbo, Mr Big Brother.

“Madhumuni ya kutoa single hii ni kuwakilisha Tanzania na muziki wetu Africa na dunia, na pia nchi zenye kupendelea kuangalia Big Brother ambao wafuatiliaji wa kipindi hicho cha miezi mitatu wako zaidi ya million 20, amesema Julio kwenye maelezo yake.


“Huu ndo muda nchi yetu itasikika kirahisi kimuziki kwa nchi 54 Africa kwasababu ya nyimbo kuwa kali na vigezo vyote na kwamba inahusiana na hiyo show. Wimbo unaitwa MR BIGB ROTHER na unaoongelea Big Brother kama show,nchi zinazoshiriki,msiba tuliopata mwaka jana heshima kutoka kwa watanzania baada ya kumpoteza mshiriki mkubwa mwaka jana Goldie,” amesisitiza Julio.
“Huu ndio mwimbo wetu kwa mara ya kwanza katika historia ya bigbrother msanii kutoka nchini kutoa mwimbo kwa ajili ya Big brother Africa na support ya watanzania itatufanya kufikisha muziki wetu nje ya Tanzania na Africa. Big Brother mwaka huu inaanza baada ya wiki mbili, 26 May. Tujivunie cha kwetu na kupeperusha bendera yetu Africa.”
Ngoma hii imetayarishwa na Timewreckordz na NK Production.Mpaka sasa Julio ameshafanya ngoma na wasanii kama Chege, Matonya, Cassim, Countryboy,Chidi Benz, Ukeme, Bskillz,Lamar,Lucci da don,Jokate,ROBZ na wengine.

Tags:

0 Responses to “Julio wa BBA Stargame aachia ngoma mpya ‘Mr Big Brother’ ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI