Friday, May 10, 2013

KESI YA MADAWA YA KULEVYA MUME WA JACK PATRICK ARUDI URAIANI

Na Imelda Mtema
MUME wa mwanamitindo maarufu hapa Bongo, Jacqueline Patrick, Abdullatif Fundikira ‘Tiff”, aliyekuwa jela ya Gereza la Keko jijini Dar alikokuwa akishikiliwa kwa tuhuma za kufanya biashara ya madawa ya kulevya, amerudi uraiani baada ya kupata dhamana.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Tiff aliachiwa kwa dhamana Ijumaa iliyopita katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusota ‘lupango’ kwa takriban mwaka mmoja.
“Ni kweli sasa hivi Tiff yuko mtaani, ametoka kwa dhamana ila kuhusiana na suala la ndoa yake amesema haipo tena, anaangalia maisha yake,” kilidai chanzo.
Katika kupata ukweli wa habari hii, mwandishi wetu alimpigia simu Abdullatif lakini hakupokea ila Jack alipopatikana alikiri zilipendwa wake huyo kuachiwa kwa dhamana.

credit- globalpublishers

Tags:

0 Responses to “KESI YA MADAWA YA KULEVYA MUME WA JACK PATRICK ARUDI URAIANI”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI