Sunday, May 12, 2013

Magaidi yaiweka Tanzania pabaya kidiplomasia



Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe akifafanua jambo Dar es Salaam,Tanzania

TANZANIA iko hatarini kuingia katika mgogoro mkubwa wakidiplomasia dhidi ya nchi za Falme za Kiarabu (UAE) na Saudi Arabia kutokana na tuhuma za kigaidi zinazo wakabili raia wa nchi hizo.

Taarifa zilizonaswa na Habarimpya.com kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya nchini na Ushirikiano wa Kimataifa zinaeleza kwamba nchini hizo zimeanza kuihoji serikali uhalali wa kuwashirikilia raia wake.

Hatua ya kukamatwa kwa raia wa nchi hizo kwa tuhuma za ugaidi uliofanyika jijini Arusha katika Kanisa Katoliki Parokia ya Olasiti nje kidogo ya Jiji hilo ulioua watu watatu na kusababisha watu zaidi ya 62 kujeruhiwa viabaya ni ishara mbaya kwa mahusiano ya kidiplomasia.


"Serikali imepokea taarifa kutoka nchi hizo ikihoji uhalli wa raia wake kukamatwa kwa tuhuma za ugaini, hatua hii inaweza kuwa mbaya zaidi endapo itabainika kwamba watuhumiwa hao si magaidi, kwani masuala ya diplomasia baina ya Tanzania na nchi hizo inaweza kuwa mbaya zaidi, tena ukizingatia kwamba serikali inapata misaada mingi kutoka nchi hizo,kutokana na mahusiano mazuri baina yetu na wao"kilisema chanzo hicho.

Taarifa hizo pia zilidhibishwa na Waziri Bernard Membe ambaye leo anakwenda jijini Arusha kufuatilia suala hilo na hasa kwa kukamatwa raia wa kigeni wakihusishwa na tukio hilo, wakiwa ni miongoni mwa watu 12 wanaoshikiliwa na polisi wakituhumiwa kuhusika na shambulio hilo lililoua watu watatu na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa.


“Ninakwenda Arusha leo ili kufahamu undani wa suala hili. Baada ya kwenda ndiyo nitakuwa katika nafasi ya kuongelea mambo haya,” alisema Membe wakati alipoulizwa jana kuhusu malalamiko ya nchi za Saudi Arabia na Falme za Kiarabu (UAE) kuhusu kukamatwa kwa raia wao. Watu wanaoshikiliwa na polisi kwa tuhuma hizi ni pamoja nja Victor Ambrose Calist (20), Mwendasha Bodaboda na mkazi wa Kwa Mrombo, Jeseph Yusuph Lomayani (18) mwendesha Bodaboda, Mkazi wa Kwa Mrombo jijini Arusha.


Wegine ni George Batholomeo Silayo (23), mfanyabiashara na mkazi wa Olasiti, Arusha, Mohamed Sulemani Said (38) mkazi wa Ilala, Dar es Salaam na Jassini Mbaraka (29) mkazi wa Arusha. Wale wanaotuhumiwa kutoka nje ya Tanzania ni pamoja na raia wa Falme za Kiarabu (UAE), Said Abdalla Said (28), Abdulaziz Mubarak (30) na Said Mohsen wakati Jassini Mbaraka (29) anatokea Saudi Arabia.

Tags:

0 Responses to “Magaidi yaiweka Tanzania pabaya kidiplomasia ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI