Wednesday, May 8, 2013
Majeruhi 7 wa mlipuko wa kanisa, Arusha wapelekwa hospitalini Muhimbili, Lugalo
Wednesday, May 8, 2013 by Unknown
Baadhi ya majeruhi wa bomu lililolipuka katika Kanisa la Parokia teule ya Mtakatifu Joseph Mafanyakazi la Olasiti, Arusha wakiwa kwenye gari maalumu la wagonjwa kwa ajili ya kupanda ndege (jana) ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na wenzao watano ili kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.
Advertisement
Shirika hilo limewapeleka wagonjwa saba na ndugu zao wanne watakaowasaidia wagonjwa hospitalini hapo.
Wagonjwa hao ni Atanasia Reginarld (14) mwanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Olasiti, Faustine Shirima (34), Gabriel Godfrey (9) mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya Msingi Lucky Vincent, Albert Njau (35) Jenipher Joachim, Apolinari Malamsha na Fatuma Tarimo.
Mkuu wa Mkoa Magesa Mulongo alisema kuwa Serikali imeamua kuwahamisha majeruhi wengine kwenye hospitali za Lugalo na Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Pia amesema wamewaleta Madaktari kutoka Jeshi la Wananchi (JWTZ) ili kusaidiana na madaktari kwenye hospitali za Arusha kwa wakati huu wanapowahitaji ili kuwahudumia majeruhi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amewasihi wadau mbalimbali wafike kwenye hospitali za Mt. Meru na St. Elizabeth ili kuona ni kwa namna gani wanaweza kusaidia majeruhi kupata matibabu sahihi. Pia akasema wamejitolea Daktari bingwa kutoka Hospitali ya Aga Khan, Dkt. Aidan Njau kuja ili kusaidiana na madaktari wa hospitali hiyo.
Source: Wavuti
Tags:
kitaifa

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Majeruhi 7 wa mlipuko wa kanisa, Arusha wapelekwa hospitalini Muhimbili, Lugalo ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.