Home
» burudani
» MSANII ROSE NDAUKA AAMUA KUTAFUTA MAWAZO YA WATOTO WA MITAANI ILI KUBORESHA FILAMU ZAKE.
Saturday, May 4, 2013
MSANII ROSE NDAUKA AAMUA KUTAFUTA MAWAZO YA WATOTO WA MITAANI ILI KUBORESHA FILAMU ZAKE.
Saturday, May 4, 2013 by Unknown
MSANII wa filamu nchini Tanzania Rose Ndauka azidi kujizolea umaarufu na kuongeza mashabiki wa aina zote kwa kuwa karibu na watoto wa mitaani hususani katika matembezi yake ya kila siku
Msanii huyo ambaye anajitahidi kujitofautisha na baadhi ya wasanii wengine wa filamu nchini kwa kuwa karibu na jamii yake kwa vitendo hususani watoto hao wa mitaani
Akizungumza jijini Dar es Salaam Ndauka alisema kuwa katika maisha yake hususani kwa kipindi hiki ambacho yeye ni supar staa anathamini watoto wa aina yote kwani hao ndio moja ya mashabiki wake
Alisema kuwa anawathamini watoto hao hali inayomsababisha kutembea kwa miguu ili kila anapokutana nao apate nafasi ya kuzungumza nao na kubadilishana nao mawazo kwa kufanya hili anaamini kuwa anaongeza mashabiki wake na kuwafanya watoto hao kuwa karibu nao
Ndauka ambaye anaamini watoto wa mitaani wanahitaji upendo wa kila mmoja anayemzunguka alisema kuwa ni jukumu lake na nafsi yake inamsukuma kufanya hivyo ili kuzidisha upendo na kuwafanya wahisi ni sehemu moja ya jamii
Aliongezea kuwa kila anapokutana na watoto hao anahisi faraja moyoni mwake kwani hiyo ni sehemu ya kitu anachokipenda na nyakati za siku ya mapumziko hutumia muda wake mwingi kutembea kwa ajili ya kuwaona watoto na kupata mawazo yao ambayo anayatumia katika kuboresha filamu zakeTOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Tags:
burudani
This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MSANII ROSE NDAUKA AAMUA KUTAFUTA MAWAZO YA WATOTO WA MITAANI ILI KUBORESHA FILAMU ZAKE.”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.