Saturday, May 11, 2013

Zitto Kabwe atoa mtizamo wa kivita Tanzania (3)

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) Zitto Kabwe akichangia hoja Bungeni hivi karibuni Dodoma, Tanzania





WAKATI Askari wa Jeshi la Polisi ikiendelea kuwahoji na kuwasaka watuhumiwa wa tukio la magaidi kulipua Kanisa la Katoliki jijini Arusha na kuuwa watu watatu ambao walizikwa jana, huku pia Jeshi hilo likitoa dau nene kwa atakayebahatika kumnasa mtuhumiwa mkuu katika tukio hilo lililo jeruhi 70, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) Zitto Kabwe ametoa mtizamo wa kivita juu ya Taifa la Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, adui anapokuja kwenye nyumba anaangalia ni wapi ambapo ni rahisi kamba kukatika. Tumeji-“expose”, tumejiweka wazi.

Leo mtu anayetaka kuishughulikia Tanzania ata-deal na udini tu. Kwa sababu anajua watanzania hivi sasa wamegawanyika katika misingi hiyo. Jana limetokea tukio Arusha, angalia kwenye mitandao ya kijamii mara moja watanzania wenyewe kwa wenyewe na ukiangalia majina ya watu wanaojadiliana wanaanza kusemana kwa dini zao.

Ndiyo hatari ambayo tumeifikia; na ndio anachokitaka adui. Atakuja, wanaitwa “Agent Provacateur”, watapiga, mtabaki mnagombana ninyi. Tukiruhusu NYUFA hizi ziendelee hatutakuwa taifa. Ni lazima sote kwa pamoja tusimame imara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, waislam na wakristo nchi hii hawana chuki kwa sababu wanaishi pamoja, ni marafiki, ni ndugu na kama ingekuwa kwa mfano waislam wanawachukia wakristo waislam wangevunja makanisa au wangechoma makanisa au wangewalipua wakristo.

Tags:

0 Responses to “Zitto Kabwe atoa mtizamo wa kivita Tanzania (3) ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI