Home
» celebrities
» Huu Ndo Ukweli Kuhusu Kuwepo Kwa Taarifa Kua Saida Karoli Kafariki Katika Ajali Ya Maji Ziwa Victoria
Wednesday, June 19, 2013
Huu Ndo Ukweli Kuhusu Kuwepo Kwa Taarifa Kua Saida Karoli Kafariki Katika Ajali Ya Maji Ziwa Victoria
Wednesday, June 19, 2013 by Unknown
Jana kumekuwepo na taarifa kutoka kwa mwanahabari, Frederick Katulanda kupitia kundi pepe la majadiliano la MabadilikoTanzania, zikiipoti kuwa mwanamuziki aliyekuwa maarufu Tanzania na Afrika Mashariki, Saida Karoli, amefariki dunia leo hii katika ajali ya kuzama kwa boti.
Kwamba, boti hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka katika kisiwa cha Goziba ilikumbwa na dhoruba ndani ya maji ya ziwa Nyanza (Victoria) na kusababisha kifo cha mwanamuziki huyo na watu wengine waliokuwa wakisafiri pamoja katika chombo hicho.
Taarifa ya Neville Meena imetoa angalizo kutafuta uhakika kwani inasemekana kuwa Saida Karoli ni mzima, yupo jijini Dar es Salaam na hajafariki dunia kama inavyoelezwa: “Nimetafuta namba yake ya simu sijaipata, ila taarifa kutoka Bukoba na ofisi ya Ofisa Utamaduni Muleba zinasema siyo kweli... kulikuwa na uvumi mwingi mjini Bukoba na Wilayani Muleba kuhusu mwanamuziki huyo kufariki lakini baadaye ikathibitika kwamba hakuwa mmoja wa abiria.” ameandika Meena.
Kuhusiana na ajali ya boti, Meena amesema, “...ni kweli kwamba kuna boti imezama katika Ziwa Victoria.”TOA MAONI YAKO HAPA
Tags:
celebrities
This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Huu Ndo Ukweli Kuhusu Kuwepo Kwa Taarifa Kua Saida Karoli Kafariki Katika Ajali Ya Maji Ziwa Victoria”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.