Saturday, June 29, 2013
JOKATE AMWANIKA MWANAUME MPYA
Saturday, June 29, 2013 by Unknown
MWANAMITINDO daraja la kwanza Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amemwanika mwanaume mpya mtandaoni huku wakiwa wamepozi katika staili ya wapendanao.
Awali, paparazi wetu alitonywa na sosi aliyeomba hifadhi ya jina lake kuwa amemuona mwanaume mpya wa Jokate katika mtandao wa Instagram.
“Nimemuona Jokate na mwanaume wake mpya lakini simjui kwa jina, kama huamini ingia kwenye mtandao wa Instagram uone mtoto wa kike alivyojiachia katika pozi za kimahaba,” alisema sosi huyo.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu aliingia kwenye kilongalonga chake na kuperuzi katika mtandao huo kisha kujionea picha hizo, haraka sana akazisevu katika simu yake.
Aidha, wadau mbalimbali waliopo katika mtandao huo walitoa maoni mbalimbali huku wengi wao wakimpongeza.
Baada ya paparazi wetu kuzitia kibindoni picha hizo, alimsaka Jokate kwa njia ya simu ili azitolee ufafanuzi.
Mwandishi: Haloo Jokate…
Jokate: Nitumie meseji nipo kwenye kikao.
Mwandishi wetu alimtumia meseji kama alivyoshauri staa huyo ambapo alimtaka amtambulishe mwanaume huyo na aeleze kama ndiye mpenzi wake mpya, hakujibu chochote.
Paparazi wetu alimtumia meseji ya pili kumsisitiza atoe majibu ndipo alipojibu kwa kifupi:“Hapana mumy!”
Pamoja na majibu hayo, paparazi wetu alimtumia meseji nyingine kumuuliza kama siyo mpenzi wake ni nani lakini hadi tunakwenda mitamboni, hakujibu chochote.
Kabla ya kumuanika mwanaume huyo, Jokate aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku pia akitajwa kutoka na mcheza kikapu, Hasheem Thabeet.
Source:Global Publisher
TOA MAONI YAKO HAPA
Tags:
celebrities ,
udaku

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 Responses to “JOKATE AMWANIKA MWANAUME MPYA ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.