Friday, June 14, 2013
Marekani imefuta safari ya Obama kuja Tanzania
Friday, June 14, 2013 by Unknown
WAKATI Serikali ya Tanzania ikiendelea na maandalizi ya
Rais waTanzania akitafakari jambokupokea msafara wa watu 700 waliotarajia kuingia nchini kwa ziara ya Rais wa Marekani Barack Obama, Rais huyo amesitisha safari yake.
Ikulu ya Marekani imetangaza kwamba msafara wa Rais Obama kuja kutembelea Bara la Afrika haitakuwepo tena,baada ya serikali ya nchi hiyo kukosa fedha itakayoweza kugaramia safari ya Rais huyo.
Taarifa iliyonaswa naHabarimpya.com kutoka katika mitandao mbalimnali nchini Uingereza na Marekani zinaeleza kwamba mbali na suala la bajeti ya Rais huyo kuja nchini Tanzania kuwa kubwa pia kamati ya sheria ,ulinzi na usalama wa Marekani imeshindwa kuthibitisha juu ya suala la ulinzi na Usalama wa Rais Obama katika kipindi chote atakachokuwa nchini Tanzania pamoja na baadhi ya nchi Barani Afrika.
Taarifa hiyo pia ilieleza kwamba msafara wa Rais Obama unahitaji maandalizi ya kutosha kwa sababu ni msafara unaohusisha watu wengi pamoja na vyombo mbalimbali vya ulinzi ikiwemo wanyama.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani alisema kwamba serikali ilijaribu kuangalia uwezekano wa Rais Obama kuja Tanzania na baadaye kutembelea Senegel pamoja na Afrika Kusini ambapo alitakiwa kukaa Tanzania kwa saa mbili tu lakini gharama za ulinzi imekuwa kubwa sana.
Nakala ya taarifa hiyo iliyonaswa naHabarimpya.com pia ilimkariri msemaji huyo wa Ikulu ya Marekani akisema kwamba pia katika msafari huo ni lazima iwe na vifaa maalum vya kutolea matibabu katika kipindi chote cha ziara ya Rais, lazima pia iwe na chombo maalum kwa ajili ya waandishi mbalimbali wa habari pamoja na vyombo vingine vya usalama kwa ajili ya kutoa taarifa ya safari ya Rais ,pamoja ndege zitakazokuwa zikizunguka kuangalia hali ya usalama katika hoteli zote atakapo kuwa ana alala Rais Obama na msafara wake.
Taarifa hiyo ilifafanua kwamba safari hiyo ndiyo safari kubwa kuliko aliyowahi kuifanya Barani Afrika ambapo alifika nchini Ghana, tangu alipochaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwaka 2009 ambapo inakadiriwa kuwa itachukua kati ya dola za marekani 60 million sawa na tsh bilioni 96,000,000,000 na dola 100 milion sawa tsh bilioni 160,000,000,000.
via Habarileo.

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Marekani imefuta safari ya Obama kuja Tanzania”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.