Home
» burudani
» Mshindi wa redd's miss nyamagana 2013 avuliwa taji hilo baada ya kubainika kuwa siyo mtanzania na alidanganya umri wake
Tuesday, June 11, 2013
Mshindi wa redd's miss nyamagana 2013 avuliwa taji hilo baada ya kubainika kuwa siyo mtanzania na alidanganya umri wake
Tuesday, June 11, 2013 by Unknown
Aliyekuwa mshindi katika shindano la kumtafuta mrembo wa wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, Redd’s Miss Nyamagana 2013 Diana Amimo amevuliwa taji hilo baada ya kubainika kudanganya umri wake pamoja na urai, kasoro zilizompunguzia sifa za kuvaa taji hilo.
Diana Amimo (katikati)
Mratibu wa shindano hilo lililofanyika (May 11) jijini Mwanza, bwana Mukhsin Mambo wa Stoppers Entertainment, ameeleza kuwa baada ya kugundua mapungufu hayo kwa Diana, kamati ilikaa (June 6) na kuamua taji hilo kumvisha aliyekuwa mshindi wa pili Rosemary Peter ambaye sasa ndio Redd’s Miss Nyamagana 2013.
Mr. Mambo amesema udanganyifu huo uligunduliwa na kuthibitishwa na idara ya uhamiaji mkoa wa Mwanza wiki moja baada ya shindano hilo, baada ya maafisa wake kumshikilia na kumuhoji mrembo huyo na kubaini kuwa Diana ni raia wa Kenya na ana umri wa miaka 17.
Kwa Mujibu wa kanuni na vigezo vya mashindano ya urembo hapa nchini, msichana lazima awe raia wa Tanzania na mwenye umri wa miaka 18 hadi 24
Tags:
burudani

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 Responses to “Mshindi wa redd's miss nyamagana 2013 avuliwa taji hilo baada ya kubainika kuwa siyo mtanzania na alidanganya umri wake”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.