Monday, June 10, 2013

Mwanalibeneke Othmani Michuzi kafanya vitu vikubwa ndani ya Kili Award



Video kamera yake a.k.a "Jicho la Tatu" imenasa kitu Demo ya Kimataifa!

Mwanalibeneke Othman Michuzi a.k.a "m2 ya mtaa kwa mta" wa Michuzi Media Group juzi alitinga ndani ya Kilimanjaro Music Award katika ukumbi wa maraha na burudani pale Mlimani City,Jiji Dar.
Alichokifanya mwanalibeneke huyo Othmani Michuzi kwa kutumia kamera yake
au Jicho Kubwa lionalo mbali ,ni kurekodi video ya matukio,ambayo video hiyo
inawezekana ikawa ndio tiketi ya kuupeperusha muziki wa Tanzania katika masoko
ya kimataifa, labda wengi walistushwa na kiwango cha juu cha kimataifa katika video


Wataalamu wa masoko wa kimataifa waliotazama video hiyo katika Youtube,wameshauri kuwa itakuwa jambo la busara kwa Michuzi Media Group,
Kuhifadhi haki yake katika video hizo, na mameneja wa wasanii au bendi wakae
meza moja na manajementi ya Michuzi Media Group,ili wakubaliane kutumia
Bidhaa hiyo kuwa Demo ya kuwaporomoti wasanii au bendi zao.
Kuzitumia bila ya ridhaa ya alipiga video ni kinyume cha sheria.
Kukopi na kupesti bila ya Idhini au ridhaa ya walipiga video hiyo ni kuvunja
sheria na heshima.
ni Ushauri,
lakini Ongera nyingi sana sana kwa Othumani Michuzi kutoka kwa wadau wa ughaibuni. https://www.youtube.com/watch?v=ZDcmpDoZQZM
Kazi imepeperusha Bongo Kimataifa endelea kwa kasi hiyo hiyo 



Libeneke lake hili http://www.othmanmichuzi.blogspot.com

Tags:

0 Responses to “Mwanalibeneke Othmani Michuzi kafanya vitu vikubwa ndani ya Kili Award ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI