Friday, June 28, 2013

MWENGE KIMENUKA , POLISI NA MGAMBO WA JIJI WASHIRIKIANA KUPAMBANA NA WAMACHINGA



Leo jioni wakati natoka katika shughuli zangu nilipita maeneo ya Mwenge pale stand ya mabasi nimekuta kweupe wale vijana wanao uza nguo kwa kupanga chini na kuzishika sikuwaona ...nikauliza nikaambiwa wamefukuzwa kwa ajili Oboma Anakuja...Mmhhh Kazi kweli kweli ...
Wakati bado nashangaa shangaa Mara likaja gari la Polisi na Wale mgambo wa jiji...Mara nikaona watu wanakimbia huku na kule ...Kushangaa kumbe wale wamachinga bado wapo ila wanauza kwa kujificha ficha kwenye vichochoro vya maduka..Sasa Kimbembe kikaanza wale wanamgambo wakawafuata huko huko na kuanza kuwapiga na kuwavunjia meza na viti vyao...Kwa kweli iliniuma sana kuona watanzania wenzetu wakifanyiwa hivyo ....Bado sijapata jibu ...siko zote mbona hawakufukuzwa ?? Huu Ugeni ndio imekuwa Nogwaaaaa....Na uhakika kuna ambao wanalisha na kutunza familia kwa kazi hizi za umachinga sasa watakula wapi kama hali ndio hiyo????

By Regina Iwole
TOA MAONI YAKO HAPA

Tags:

0 Responses to “MWENGE KIMENUKA , POLISI NA MGAMBO WA JIJI WASHIRIKIANA KUPAMBANA NA WAMACHINGA ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI