Monday, July 1, 2013
Barabara Ya Mitaa Ya Ubungo ikiwa Inapigwa deki Ili Jiji Lionekane Safi
Barabara Ya Mitaa Ya Ubungo ikiwa Inapigwa deki Ili Jiji Lionekane Safi Wakati Obama akienda Ubungo. Ni Usafi wa hali ya Juu.
Kinachoonekana sasa hivi ni taswira ya Taifa "tunapenda tuoekane" wasafi kumbe ili Obama atuone tuko Wasafi hali hii inanikumbusha enzi za Ujana wetu, Wakati Huo unajinyima hela Ili ukanunue Perfume "tuonekane" kwetu kuna Uwezo, nakumbuka ilikuwa tunaenda Kukopa hela kwa Washikaji Ili Tumtoe "binti" outing, unakuta Mtu ananunua simu ya gharama ili "aonekane" kuwa nae wamo, nakumbuka enzi hizo Kulikuwa kuna wadada ikitokea kuna kasherehe ama outing mtu anaenda azima nguo ili "aonekane" mambo fulani.
Wakati tunasoma kulikuwa na watu wanaingia na "MIGI" wengine "Vibomu" ama "Simbi" ili "waonekane" wamefaulu. Nimewahi kukutana na watu wenye madeni makubwa kwa sababu tu walinunua flat screen, wakanunua na gari na carpet ili "waonekane" kuwa wako vizuri. Kuna watumishi wa mungu ambao wao kaw kutaka "kuonekana" wana Upako wameenda kutafuta nguvu za uchawi.
Kuna watu ambao kwa sasa wana ndoa za Majuto kwa sababu walitaka "kuonekana" na watu kua nao wanandoa, Kuna watu ambao walienda Kupanga nyumba maeneo fulani ili waonekane mambo safi kumbe walijinyima miezi 700 ili wakae hapo.
Kiwango cha "kuonekana" kinakufanya upewe sifa isiyo yako, unataka watu wakuone wewe ni "A" kumbe wewe ni "B", unataka uonekane mambo safi kumbe wewe ni kama mimi tu, Unataka Uonekane wewe Mji wako ni Msafi Kumbe ni Mchafu kama kawaida. Tunachokiona Kinafanyika ni Taswira Ya Taifa Tulililonalo, Ni Taswira ya Familia tulizonazo ni Taswira ya Maisha Ya Watanzania...Sishangai sana.
Niko Busy Kumpokea Obama
by FUNUNU HABARI REPORER-SAmsasali.

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
0 Responses to “Barabara Ya Mitaa Ya Ubungo ikiwa Inapigwa deki Ili Jiji Lionekane Safi ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.