Thursday, September 26, 2013

CHADEMA yapata pigo kubwa wilayani Handeni.Mwenyekiti, katibu na wanachama 380 wahamia CCM





Uongozi wa juu wa Chama Cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya 
Handeni Mkoani Tanga umekihama Chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wa 
Wilaya na Katibu wake pamoja na wanachama 380 ambao wamejiunga na Chama 
Cha Mapinduzi (CCM)..

  

Tukio hilo linalotoa taswira mbaya kwa CHADEMA  na ishara njema kwa CCM 
limetokea juzi katika kata ya Kwamatuku, ambapo Mwenyekiti wa jumuiya ya
Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdallah Bulembo alifanya mkutano 
wake wa hadhara na kupokea wanachama hao wapya wa CCM kutoka CHADEMA.

  


Viongozi hao wa Chadema ni pamoja na Mwenyekiti wa wilaya ya handeni, 
Luka Selemani, mwenyekiti wa kitongoji cha maguruwe, mjumbe wa Baraza 
Kuu Taifa (Chadema) na Mwenyekiti wa kamati ya utendaji ya wilaya. 



Wengine ni Katibu wa wilaya hiyo, Athumani Ngido ambaye pia ni mjumbe wa
baraza kuu Taifa na mwenyekiti wa kamati ya utendaji wa Mkoa wa Tanga.,
Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya wilaya hiyo, Jack son Fransis ambaye 
pia ni mwenyekiti wa kata ya Kabuku na mgombea udiwani wa Kata hiyo...

  


Mbali na hao, wamo Mwenyekiti wa Tawi la umoja wa Vijana wa Tawi la 
Kwamatuku, Abrahaman Mtengwa na mjumbe wa kushughulikia migomo ya chama 
hicho, Juma Mkomba..  

  

Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara, Bulembo alisema kukimbia 
kwa viongozi na wanachama hao ni ishara kuu ya chama hicho kusambaratika
vipande vipande katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu... 

  

Alisema kadiri siku zinavyokwenda Chadema kitazidi kusambaratika 
kutokana na baadhi ya viongozi wake kukumbatia madaraka huku wengine 
wakiachwa kuwa wapiga debe.

Tags:

0 Responses to “CHADEMA yapata pigo kubwa wilayani Handeni.Mwenyekiti, katibu na wanachama 380 wahamia CCM”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI