Tuesday, September 10, 2013

MATANUZI YA KUFA MTU.., KUMBE ILIKUWA JEURI YA MADAWA YA KULEVYA



Siku nyingi nilikuwa najiuliza hawa Watanzania wenzangu wanapata wapi pesa za kutesa namna hii? Nilikuwa nashangaa nikitoka out usiku nikiwa nimejidundulizia vipesa vya mtoko kwa zaidi ya miezi sita tena kwa kujibana ajabu, cha kushangaza naenda kujionea jinsi watu wanavyojirusha kwa ufahari wa hali ya juu. Matumizi yao ni kufuru, magari waliyopaki nje ya kumbi za starehe ni ya gharama nisiyoweza kuifikiria! Bei ya mavazi waliyovaa ndio usiseme.

Nikifikiria elimu ya watoto wangu, uwiii nachanganyikiwa! mbona wa TZ wenzangu wanapeleka watoto wao kwenye mashule ya gharama ambazo mimi niliziona kama kufuru! mmmh kwani hawa wenzangu wanapata wapi hayo manoti yote? mbona mie siyapati? kama ni mshahara huu huu tena kuna wengine nawazidi mshahara, kama ni bajeti; sidhani kuna anayenifikia kwa kujua kubana matumizi. Kama ni biashara ... mmmh sijaona ya kuwafanya watu wawe hivi... sana sana naona mabutiki yanafunguliwa tuuuuuu na hayana wateja... mashoo room yamesambaaa kila kona sioni wanunuzi, labda biashara ya mabar na glossary naweza sema yanalipa. sasa inakuwaje? Loooh nimeanza kufunguka sasa kumbe wengi wao walikuwa wanashiriki kwa namna moja au nyingine kwenye hii biashara ya DAWA! 

Biashara iliyopandisha maisha ya Watz kuwa ya juu na kutengeneza matabaka maana imetufanya wengine tuonekane kama hatujui kutafuta pesa na hatujui mipango... Looo umefika wakati wao wa kuumbuka sasa.... naanza kuona dalili za kukosekana kwa wateja kwenye mabaa na maclub, magari ya kifahari kupungua barabarani, makanisani, masherehe na sehemu mbalimbali za starehe! mmmmmm naendelea kusikilizia majina yanayotajwa huko kwenye ushiriki wa madawa! mboni mambo!! masikio yanaanza kuwasha maana tutasikia hata tusiyoyatarajia.....

WaTz kiboko! hadi mnakodi meli??? du kumbe nchi hii imeshaoza eeeeeeeh! Ona hospitali zinavyojaa waathirika wa madawa, cheki vituoni ujionee mateja yanavyonesa ..... balaa hili. 

EEE MUNGU WAUMBUE WOTE NA BIASHARA HII IFE KIFO CHA MENDE, WATOTO WETU WAPONE; AMENI.

Tags:

0 Responses to “MATANUZI YA KUFA MTU.., KUMBE ILIKUWA JEURI YA MADAWA YA KULEVYA”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI