Saturday, February 22, 2014
AUNT EZEKIEL AANGUKA KWA PRESHA, ALAZWA. SOMA KISA HAPA
Staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel.
STAA wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuanguka ghafla kwa presha akiwa ‘location’ jijini Tanga, Risasi Jumamosi lina habari hii.
Kwa mujibu wa chanzo, Aunt akiwa katika harakati za kuigiza filamu anayocheza na Amri Athuman ‘Mzee Majuto’, ghafla alianguka na kukimbizwa katika Hospitali ya Gesha jijini humo.
Aunt Ezekiel akiwa hospitali amelazwa.
Baada ya kuzipata habari hizi, mapaparazi wetu walimtafuta Aunt kwa njia ya simu na alipopatikana alikiri kuanguka kutokana na kusumbuliwa na presha ya kushuka.
“Kweli nilikuwa shutting na Mzee Majuto, ghafla nilianguka na kukimbizwa hospitali, wameniwekea dripu mkononi ila namshukuru Mungu, naendelea vizuri,” alisema Aunt
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
0 Responses to “AUNT EZEKIEL AANGUKA KWA PRESHA, ALAZWA. SOMA KISA HAPA”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.