Friday, February 28, 2014
TANGAZO_LA_USAILI_NAFASI_YA_MLINZI
Friday, February 28, 2014 by Unknown
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/E/41 26 FEBRUARI, 2014
KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anatarajia kuendesha usaili kwa waombaji kazi wa Tangazo la tarehe 27 Novemba,2013 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi, waombaji kazi watakaofaulu usaili.
Kila mwombaji aliyekidhi vigezo na kuchaguliwa kwa ajili ya usaili anapaswa kwenda kufanyia usaili katika mkoa aliopangiwa kama anwani yake inavyoonesha katika tangazo hili.
Wasailiwa wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
1. usaili utaanza na ukaguzi wa vyeti halisi saa moja kamili asubuhi(1:00) na utafanyika mahali na tarehe kama inavyoonesha katika nafasi husika, Wasailiwa hawaruhusiwi kubadilisha kituo cha usaili.
2. Kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha mkazi, kupigia kura, kazi, hati ya kusafiria n.k
3. Kuja na Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne, sita, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji.
4. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
5. Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
6. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
7. Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa usaili
8. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
9. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA)
10. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba tena mara nafasi za kazi zitakapotangazwa.
11. Kada zenye mchujo, wasailiwa watakaofaulu mtihani wa mchujo wazingatie mahali na tarehe za usaili wa mahojiano kama ilivyooneshwa kwenye tangazo.
******************DOWNLOAD HAPO CHINI******************
www.jobsonlinetz.com

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TANGAZO_LA_USAILI_NAFASI_YA_MLINZI”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.