Friday, February 21, 2014
NJIA SAHIHI ZA KUIFANYA NGOZI YAKO KUWA VIZURI NA KUONDOA MAFUTA
Friday, February 21, 2014 by Unknown
KILA msichana ana ndoto ya kuifanya ngozi yake kutelezea na kuwa katika hali nzuri yenye kuleta mvuto. Hapa nitakupatia njia nzuri itakayofanikisha hilo.
Ndizi na maziwa
Chukua ndizi, changanya na maziwa kisha paka uso wako mpaka kwenye shingo .
Mchanganyiko huu utafanya uso wako kuvutia na kutelezea. Mbali na hilo, mkorogo huu utasaidia kukuza ngozi yako na kuondoa ngozi iliyokufa.
Asali na maziwa mtindi
Chukua asali, changanya na maziwa mgando kisha paka kwenye uso wako. Kaa na mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 15, pia unaweza kuchanganya asali na limao. Unaweza kupaka mchanganyiko huu kila siku.
Chembechembe za mkate na cream ya maziwa
Chukua mkate, uchambue chambue kupata chembechembe kisha changanya kwenye cream ya maziwa ili kupata ngozi inayoteleza na kuondoa makunyanzi.
Viazi mbatata pekee au na nyanya
Viazi mbatata na nyanya unaweza kutumia kila kimoja peke yake kupaka usoni na kuleta ngozi nzuri, unaweza kutumia urembo huu kila siku hauna madhara.
Mbegu za alizeti na maziwa
Ukishachanganya mbegu hizi kwenye maziwa, paka muda wa jioni, mchanganyiko huu unaweza kuuchanganya na bizari kidogo. Mchanganyiko huu utakusababishia ngozi yako kuwa ya kiasili zaidi.
Ute mweupe wa yai na asali
Paka ute mweupe wa yai na asali, kaa kwa muda wa dakika 20. Mchanganyiko huu utaifanya ngozi yako kukakamaa na kuvuta ngozi lakini utakusaidia kulainisha na kukufanya uonekane mdogo
Maoni yako
Tags:
fashion

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NJIA SAHIHI ZA KUIFANYA NGOZI YAKO KUWA VIZURI NA KUONDOA MAFUTA”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.