Monday, March 18, 2013
KWETU PAZURI KUZINDUA ALBAMU DAR PASAKA
Monday, March 18, 2013 by Unknown
KUNDI la muziki wa kiroho la Ambassadors of Christ ‘Kwetu Pazuri’ la Kigali, Rwanda linatarajia kuzindua albamu yao mpya iitwayo Kaeni Macho Machi 31 mwaka huu Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema Dar es Salaam jana kuwa kundi hilo limemuhakikishia kwamba albamu hiyo itakuwa moto wa kuotea mbali na kuzitaja nyimbo zilizopo katika albamu hiyo kuwa ni Kaeni Macho, Mungu Wangu, Tugireurukundo, Ewe Ndugu, Tuombeane, Umwamini Yesu, Msalaba, Twawona, Okuswala na Huruma.
“Kundi hilo maarufu kwa jina la Kwetu Pazuri limefurahi sana kuja hapa Tanzania na wamenieleza albamu hiyo hawajawahi kuizindua hivyo ni baraka kubwa kwa Watanzania kupewa heshima hiyo,” alisema Msama na kuongeza kuwa kundi hilo pia litatumbuiza katika maonesho mengine ya mikoani.
Kwa mujibu wa Msama hivi sasa kundi hilo linatamba na albamu ya Mtegemee Yesu na wamemuhakikishia kuwa watang’arisha tamasha la mwaka huu na wamejipanga vya kutosha kuhakikisha mashabiki wanapata burudani ya nguvu.
Alisema albamu yao hiyo ina nyimbo nane ambazo ni JY’ Ushima Uwite, Mtegee Yesu, Ndifuza Kugerayo, Iyana Iby’ Isi, Yesu Niwe Mungeri, Parapanda, Abasaruzi na Nenda.
Licha ya kundi hilo, wasanii wengine wa nje ya Tanzania watakaotumbuiza tamasha hilo ni Sipho Makhabane wa Afrika Kusini, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya. Wasanii wa Tanzania waliothibitisha hadi sasa ni Rose Muhando, Upendo Nkone, John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival na kundi la Glorious Celebration
Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31 na litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Tags:
burudani

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KWETU PAZURI KUZINDUA ALBAMU DAR PASAKA ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.