Tuesday, March 12, 2013
MWANASIASA MKONGWE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU ASISITIZA MATUMIZI YA KISWAHILI
Tuesday, March 12, 2013 by Unknown
…………………………………………………………….
MWANASIASA mkongwe nchini Kingunge Ngomble Mwilu amewataka Watanzani kuienzi Lugha ya Kiswahili kama nyenzo itakayosaidia katika kukuza na kuleta maendeleo katika elimu nchini.
Kingunge aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abed, kilichoandikwa na Mathias Eugen ambapo uzinduzi huo uliandaliwa na familia ya Kaluta na baadhi ya wataalamu wa lugha hiyo kutoka Bakita.
Alisema anathamini uzinduzi wa kitabu hicho ambacho kimekusanya kazi mbalimbali zilizofanywa na Hayati Kaluta wakati wa uhai wake.
Kingunge alisema kila Taifa duniani ili liweze kupiga hatua mbalimbali za maendeleo ni lazima liwe na lugha inayofahamika vizuri na raia wake ambapo kwa Tanzania rugha rasmi ni Kiswahili.
“Lugha ni chombo cha msingi kwa binadamu pia inatofautisha kati ya binadamu na viumbe vingine ambapo kupitia lugha ndipo tunapokuza uwezo wa kufikiri kwani huwezi kukuza uwezo wa kufikiri biala ya kuwa na lugha ya kueleweka”alisema Kingunge.
Aidha, aliwapongeza akina Hayati Kaluta na wenzake kwa kuiheshimu lugha hiyo ambayo mara zote imekuwa ikitumika katika kujenga umoja wa taifa hilo.
Aliwasa Watanzani kuacha tabia ya kukifanya Kiswahili kuwa ni tatizo na baadala yake kuwandaliwe mikakati ya lugha hiyo ili iwe ya kufundishia katika vyuo vikuu nchi lengo likiwa kujenga uelewa mzuli wa lugha, inayozungumzwa hata kwenye Umoja wa Mataifa (UN).
Miongoni mwa watu maarufu waliohudhuria katika uzinduzi huo ni pamoja na Balozi Job Lusinde, Suleiman Hega, Hashim Mbita na wengine ambapo wote, kila mmoja alisistiza matumizi ya lugha hiyo kwa ufasaha.

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWANASIASA MKONGWE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU ASISITIZA MATUMIZI YA KISWAHILI”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.