Tuesday, March 12, 2013

MANISPAA YA KINONDONI KUKUSANA BILIONI 156 2013/2014





MANISPAA ya Wilaya ya Kinondoni inatarajia kukusanya zaidi ya sh bilioni 156 kwa ajili ya matumizi ikiwa ni pamoja na kuendeleza miradi ya maendeleo katika manispaa hiyo kwa mwaka wa fedha 2013/2014.
Akizungumza wakati wa kupitisha bajeti Manispa hiyo, jijini Dar es Salaam jana,
Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda alisema kuwa fedha hizo zinatarajiwa kukusanywa katika vyanzo mbalimbali vya mapato katika manispaa hiyo ikiwa ni pamoja na michango ya wananchi na ruzuku kutoka serikali kuu.

“Wakurugenzi mlipata shida sana wakati wa kupitisha bajeti hii kwa waheshimiwa madiwani lakini hiyo yote ni kwa ajili ya kujenga halmashauri ya manispaa ya Kinondoni wananchi wanahitaji kuona maendeleo na kuwa na bajeti yenye vipaumbele muhimu katika manispaa,”alisema Mwenda.

Mwenda alisema kati ya fedha hizo sh bilioni 49.2 zinazotarajiwa kutokana na mapato ya ndani huku sh bilioni 1.5 zitakuwa ni michango ya wananchi, ambapo serikali kuu imetoa ruzuku ya sh bilioni 91.1 na sh bilioni 15 zitatolewa na benki ya CRDB kwa ajili ya upimaji wa viwanja vya Mabwepande.

Alisema katika sh bilioni 91.1 za ruzuku kutoka serikali kuu, sh bilioni 66.4 ni kwa ajili ya mishahara, sh bilioni 8.3 ni matumizi ya kawaida na sh bilioni 16.2 ni ruzuku ya miradi ya maendeleo.
Aliongeza kuwa bajeti ya mwaka 2013/2014 ni mwendelezo wa halmashauri kutekeleza Malengo ya Milenia na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025.
Naye diwani wa Sinza Renatus Pamba (Chadema), alisema bajeti hiyo imepita bila kupigwa na wajumbe kutokana na bajeti kuwa shirikisha ambapo fedha nyingi zimetengwa kwa ajili ya kusaidia wananchi kwa kuziweka katika miradi ya maendeleo.

“Bajeti ya mwaka huu ni ya kihistoria katika manispaa ya Kinondoni tofauti na tulivyoikuta tumekaa katika kikao kwa kutengwa katika kamati mbalimbali kuijadili kwa muda wa siku tano,fedha zilizokwenda kwenye miradi ya maendeleo ni nyingi ambazo zitasaidia kuendeleza manispaa,”alisema Pamba.

Tags:

0 Responses to “MANISPAA YA KINONDONI KUKUSANA BILIONI 156 2013/2014”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI