Tuesday, March 12, 2013
Sleiman Seif Omar awataka wanahabari kufanya utafiti wa kina kuhusu habari zao
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
Meneja wa Baraza la Habari kanda ya Zanzibar Suleiman Seif Omar ( Bin Seif) amewataka waandishi wa habari kufanya utafiti wa kina katika habari wanazoziandika kama zina ukweli na uhakika.
Hayo aliyasema jana wakati akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali katika ukumbi wa Mansoon Hotel Vuga
Alisema waandishi wa habari wanapokuwa kazini wawe makini kuandika habari zinazozingatia maadili yote ya habari ikiwemo ukweli na uhakika.
Alisema kuandika habari kwa kuzingatia vigezo hivyo kunamuwezesha mwandishi kuwa muadilifu na kujiamini katika kazi yake.
Alisema Baraza la Habari Tanzania kazi yake ni kushajihisha waandishi wa habari na kuiwapa muongozo jinsi wa utafutaji wa habari na kuziandika vyema ili ziwafikie wananchi wa taifa hilo .
“Kila mtu ana haki ya kupata habari ila habari hizo ziwe za ukweli na uhakika hivyo mwandishi nalazimika kuzifanyia utafiti wa kina habari anazozipata kabla ya kuziwasilisha kwa wananchi kupitia chombo cha habari”. Alisisitiza Bin Seif.
Meneja huyo aliwaambia waandishi wa habari wawe watafiti wa habari na matukio ili kuziwasilisha kwa wananchi kama tukio hilo lilivyotokea.
Nae mwandishi wa BBC Ali Saleh (Alibato ) alisema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kujifunza zaidi ili kuepukana na makosa ambayo hayastahiki kujitokeza na kuitia aibu fani hiyo.
“Habari zipo lakini waandishi wa habari hakuna kutokazana na kutoweza kujifunza kusoma makala, vitabu pamoja kutosikiliza habari mbali mbali za ndani na nje ya nchi”. Alisema Ali Saleh.
Nao waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo walisema hakuna uhuru wa kutosha katika kutoa habari jambo ambalo linawajengea hofu na kutokujiamini katika kazi zao .
Mkutano huo wa siku moja kwa Waandishi wa Habari umeandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) ambao umebeba mada Haki ya Kupata Habari

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
0 Responses to “Sleiman Seif Omar awataka wanahabari kufanya utafiti wa kina kuhusu habari zao”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.