Sunday, March 24, 2013
ULIMWENGU, SAMATTA WANG’ARA STARS IKIITUNGUA MOROCCO TATU
Sunday, March 24, 2013 by Unknown
Timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mechi ya awali kuwania kucheza Kombe la Dunia.
Stars imefanikiwa kuibuka na ushindi huo mnono baada ya kuwachapa Morocco katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Stars yamefungwa na Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta, wote wawili ni washambuliaji wa TP Mazembe ya DR Congo.
Pamoja na kuifunga Morocco, kikosi cha Stars chini ya Kocha Kim Poulsen kilitawala mchezo kwa muda mwingi na mashabiki walionyesha uzalendo kwa kuwashangilia mwanzo mwisho.
Stars iko katika kundi moja na Ivory Coast, Gambia na Morocco na ushindi huo umewafanya wakae kileleni mwa kundi hilo.
CREDIT- SALEH JEMBE
Tags:
burudani

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ULIMWENGU, SAMATTA WANG’ARA STARS IKIITUNGUA MOROCCO TATU”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.