Friday, April 5, 2013
BARCELONA YAWATUMIA LIONEL MESSI NA MESCHARANO KUMUALIKA PAPA KWENDA NOU CAMP
Friday, April 5, 2013 by Unknown
Mkuu huyo wa kanisa katoliki, Papa Francis, ni shabiki wa klabu ya nyumbani kwao San Lorenzo na amekuwa akizivutia timu nyingi tangu alipochaguliwa kuwa Papa mwezi uliopita.
Mastaa wa Argentina kama mshindi wa mara nne wa Ballon d’Or Lionel Messi na mchezaji wa zamani wa Liverpool Javier Mascherano kwa sasa wapo kwenye kikosi cha Blaugrana, na Rosell anasema litakuwa jambo la maana ikiwa mkuu huyo wa Wakatoliki kuweza kuhudhuria mechi mojawapo ya Barca.
Alisema kwenye barua iliyochapishwa na gazeti la El Mundo Deportivo: "Kama Raisi wa Barcelona na itakuwa jambo la heshima kubwa kushea na wewe kitu ambacho wote tunakipenda nacho ni mchezo wa soka.
"Ningependa kukaribisha kuangalia mechi kwenye dimba la uwanja wa Camp Nou na kufurahia mchezo wa soka kutoka kwa wachezaji wetu, hasa waargentina wenzioMessi na Mascherano, ambao wamesapoti mualiko huu kwa kuweka saini zao kwenye barua hii.”
CHANZO SHAFIH DAUDA
Tags:
burudani ,
michezo
This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BARCELONA YAWATUMIA LIONEL MESSI NA MESCHARANO KUMUALIKA PAPA KWENDA NOU CAMP”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.