Saturday, April 6, 2013

Beef kati ya T.I.D na Ommy Dimpoz? Kilichotokea Maisha Club jana usiku ndio hiki




kama umekua ukiwafatilia hawa mastaa wawili, stori kwamba hawapatani toka Ommy Dimpoz alipoondoka Top Band itakua sio mpya kwako.

Ommy ameripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwa muda mrefu kutokua na uhusiano mzuri na T.I.D toka alipotoka kwenye hiyo band.

T.I.D Ommy na Mwisho Mwampamba.

Baada ya hayo yote, jana April 5 2013 T.I.D akiwa Maisha Club sehemu ya V.I.P alimuita Ommy Dimpoz na kupiga picha ya pamoja kabla ya kuongea na millardayo.comna kufuta sumu iliyoenezwa kwenye headlines kwa kipindi kirefu.

Kwenye interview hiyo ambayo itasikika pia kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM jumatatu April 8 2013, T.I.D amesema “watu wengi wananiona mimi ni Mkorofi lakini niko tofauti sana na wanavyofikiri, sikuwahi kuwa na ugomvi na Ommy, nimekaa nae kwa miaka minne….. taarifa za beef ni za watu tu walioamua kuniharibia tu lakini niko poa na Ommy”

Tags: ,

0 Responses to “Beef kati ya T.I.D na Ommy Dimpoz? Kilichotokea Maisha Club jana usiku ndio hiki”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI