Sunday, April 14, 2013

Kati ya CHADEMA, CCM na BUNGE, Nani Ameingilia Uhuru wa Mahakama?



Wadau, baada ya tukio la kukamatwa Lwakatare na hatimaye kufikishwa mahakamani kutokana na kutuhumiwa kupanga njama za kigaidi, mjadala mkali umeibuka hapa nchini na viongozi wa CHADEMA na CCM mara kadhaa wamesikika wakishutumiana katika tukio hilo la Lwakatare. Bila kujali kuwa kesi hiyo ipo mahakamani, viongozi wa chademawamesikika wakitamka wazi kuwa chama kimoja kinahusika na tukio hilo. Mathalan chadema wanasema kuwa tukio la lwakatare ni mpango kabambe ulioasisiwa na ccm na kutekelezwa na baadhi ya viongozi na wafuasi wa chadema kwa kujua au bila kujua. Pia viongozi wa chadema wamevishutumu vyombo vya dola katika tukio hilo.maidha, kwa nyakati tofauti, chadema wameitisha press conference kuelezea tukio hilo la lwakatare na kuwashutumu waziwazi baadhi ya viongozi wa ccm hususan Naibu Katibu Mkuu, Mwigulu NchEmba kuhusika na sakata hilo

aidha, wakati akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani kwenye hotuba ya bajeti ya waziri mkuu, kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, freeman mbowe alishutumu waziwazi ccm na nchemba katika sakata hilo. Naye mwanasheria wa chadema tundu lissu pia aliungana na kiongozi wake, freeman mbowe kuelekeza lawama kwa ccm wakati akichangia hotuba ya waziri mkuu.

sambamba na hilo, baadhi ya viongozi wa ccm katika hali iliyotafsiriwa kuwa ni kujibu mapigo ya chadema, wamesikika wakitamka kuwa chadema wanajihusisha na matukio ya kigaidi na kwamba wanatakiwa kuwaomba radhi wananchi ili kujisafisha. Viongozi hao ni naibu katibu mkuu, mwigulu nchemba na katibu wa itikadi na uenezi, nape nnauye.

kwa upande wa Bunge, kitendo cha spika, Anna Makinda kuruhusu kiongozi wa upinzani kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani juu ya tukio la lwakatare kimetafsiriwa kuwa ni bunge kuingilia uhuru wa mahakama. Aidha, spika pia awaruhusu nchemba na lissu kujadili suala ambalo lipo mahakamani

kutokana na hali hiyo, je nani kati ya chadema na ccm chanzo cha kuingilia uhuru wa mahakama? Je kitendo cha bunge kuruhusu mijadala katika mambo yaliyopo mahakamani ni kuingilia uhuru wa mahakama?

je ni sahihi pia kufuta mashitaka ya lwakatare kutokana na kuingiliwa huko kwa mahakama? Je kitendo cha kuifuta kesi hiyo kwa kuhofia lawama za kisiasa si kuingilia uhuru wa mahakama?

Tags: ,

0 Responses to “Kati ya CHADEMA, CCM na BUNGE, Nani Ameingilia Uhuru wa Mahakama?”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI