Thursday, April 11, 2013

MAHACKER WAIOBOMOA WEBSITE YA PROFESA JAY.....TEMBELEA UJIONEE





Watu wanaosadikika kuwa ni wahuni wa kitechnolojia wameonekana kutenda mambo yao katika Official website ya Daddy wa muziki wa rap Tanzania, Proffesa Jay http://www.professorjaytz.com/ ambayo kwa mujibu wake mwenyewe, site hii ilikuwa bado ipo katika matengenezo na kuna mtu maalum ambaye alikuwa amemuasign kazi ya kuitengeneza.



Hivi ndivyo site ya msanii huyu inavyoonekana kwa sasa;



Jay mwenyewe ambaye hadi wakati tuliokuwa tunaongea naye alikuwa hafahamu kuhusiana na kutokea kwa issue hii, amewaahidi mashabiki wake kulifuatilia swala hili na kuhakikisha anaweka kila kitu katika mstari.

Rapa huyu mchana wa leo atakuwa akitoa Burudani pande za Chuo kikuu Cha Dar es Salaam katika Kongamano maarufu la Kigoda Cha Mwalimu Nyerere kwa mwaka huu, Kongamano ambalo limeanza jana na linatarajiwa kuisha siku ya kesho likiwa na kauli mbiu 'Maendeleo ni Mapambano ya Ukombozi'.

Tags: ,

0 Responses to “MAHACKER WAIOBOMOA WEBSITE YA PROFESA JAY.....TEMBELEA UJIONEE ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI